Header Ads

header ad

SERIKALI YATENGA BILIONI 14.5 KUPUNGUZA VIFO VINAVYOTOKANA NA UGONJWA WA SARATANI.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetenga sh bilioni 14.5 katika mwaka huu wa fedha kwa ajili ya kununua PET/CT Scan ambayo itapunguza asilimia 60 ya wagonjwa wa saratani waliokuwa wanapelekwa nje ya nchi kwa uchunguzi wa matibabu.

Akizungumza katika matembezi ya hisani ya kuhamasisha uchunguzi na kuongeza uelewa wa ugonjwa wa saratani ya matiti yaliofanyika leo jijini Dar es Salaam, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amesema serikali imejipanga kudhibiti saratani.



 Mhe. Mwalimu amesema kuwa kuongezeka kwa wagonjwa wa saratani ya matiti kumeifanya serikali kuanza utekelezaji wa mkakati wake wa kitaifa wa kudhibiti na kuzuia saratani.

Amesema kuwa juhudi mbalimbali za kuimarisha utoaji wa tiba zinafanywa kwa kuongeza bajeti ya dawa na vitendanishi kutoka shilling Milioni 790 kwa mwaka 2015/2016 hadi Shillingi bilioni 7 kwa mwaka 2016/2017 na Shillingi bilioni 7 kwa mwaka 2017/2018.
Wadau mbalimbali wakiwa katika matembezi ya hisani 
ya kuhamasisha uchunguzi wa saratani ya matiti

Hii imeongeza upatikanaji wa dawa za saratani kutoka asilimia 5 hadi 80 kwa mwaka 2017/18, juhudi hizi zimelenga kuongeza vifaa tiba vipya vya kisasa vya kutibu saratani” amesema Mhe. Mwalimu.
Imeeleza kuwa bila mchango wadau katika juhudi za kutokomeza ugonjwa wa saratani ya matiti, serikali pekee haiwezi kufanikiwa hivyo nguvu zaidi zinaitajika ili kuweza kudhibiti ugonjwa wa saratani.

Imeeleza kuwa bila mchango wadau katika juhudi za kutokomeza ugonjwa wa saratani ya matiti, serikali pekee haiwezi kufanikiwa hivyo nguvu zaidi zinaitajika ili kuweza kudhibiti ugonjwa wa saratani.

Licha ya juhudi za serikali na wadau mbalimbali katika kuimarisha huduma za uchunguzi na tiba katika hospital za rufaa na taasisi ya Saratani ya Ocean Road zipo changamoto kadhaa ambazo zimekuwa kikwazo katika kufikia malengo.
Miongoni mwa changamoto hizo ni pamoja na dhana potofu kuwa saratani haitibili, Uchache wa wahudumu wa afya hasa wataalamu waliobobea katika kufanya uchunguzi wa saratani ya katika hospitali za mikoa na wilaya.

Hata hivyo uchache na uchakavu wa mashine za kutibu saratani ukilinganisha na ongezeko la wagonjwa pamoja na ukosefu wa program mahsusi ya uhamasishaji wa wananchi kuhusu saratani ni miongoni mwa changamoto.

Takwimu za ugonjwa wa saratani ya matiti zimebainisha kuwa vifo vitokanavyo na saratani hiyo inatarajiwa kuongezeka na kufikia milioni 24 ifikapo mwaka 2035 kama juhudi za kuzuia na tiba hazitaimarishwa katika nchi zote zenye uchumi wa kati.

Hata hivyo takwimu zilizotolewa na Shirika la Afya duniani (WHO) zikionyesha ongezeko la wagonjwa wapya 14.1 milioni kila mwaka wanagundulika huku na wagonjwa 8.8 hufariki dunia.

Athari za kiuchumi zitokanazo na ugonjwa wa saratani ni kubwa na zinaongezeka kila mwaka ambapo mwaka 2010 zilikadiliwa kufikia dola za kimarekani trilioni 1.16.

Takwimu zinaonesha kuwa wanawake duniani kote, saratani ya matiti ndiyo iliyoongoza kwa kuwa na wagonjwa wapya milioni 1.7 kila mwaka wanagundulika ikilinganishwa na wagonjwa laki tano wanaogundulika na saratani ya shingo ya kizazi.

Hata hivyo matembezi ya mwaka huu yamekuwa na mafanikio makubwa ikilinganisha na mwaka uliopita na hali hii inatokana na juhudi za serikali katika kupambana na ugonjwa wa saratani.

Taasisi ya Saratani Ocean Road kwa kushirikiana na Hospital ya Aga Khan pamoja na Hotel ya Kunduchi beach imefanikiwa kuandaa matembezi ya hisani yaliofanyika leo.

Matembezi hayo yameanzia katika taasisi ya saratani ya ocean road kunazia saa 12:30  asubuhi na kuhitimishwa saa 4:00, huku mgeni rasmi akiwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Mhe Ummy Mwalimu.

No comments

Powered by Blogger.