"SIJABEBWA NA UVCCM BALI UWEZO WANGU NDO UMEFANYA NIPEWE NAFASI NILIYONAYO KWA SASA"JOKATE
Na James Bayachamo-SalvaNews
\
Mwanamitindo Joketi Mwegelo ambaye kwa sasa ni Kaimu Katibu wa uhamasishaji wa Umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM ) amekanusha uvumi unaosambaa kwenye mitandao ya kijamii nchini kuwa amepewa nafasi hiyo kwa upendeleo yani kwa kubwebwa na Mwenyekiti wa UVCCM.
"Unajua mimi nimejitoa sana kwa jamii yangu na kazi yangu
inaonekana na jamii na wala siyo ya kificho hivyo nimepewa nafasi hii
kutokana na kujitoa kwangu kuitumikia jamii"amesema Jokate mbele ya
waandishi wa habari waliomuuliza kuhusu uvumi huo.
Katika hatua nyingine Uvccm yawaasa vijana kujitokeza kwa wingi April 26 katika maadhimisho ya miaka 53 ya muungano mjini Dodom.
Hayo yamesemwa hivi leo na umoja wa vijana wa
chama cha ccm Jijini Dar es salaam wakati walipokuwa wakizungumza na
waandishi wa habari Ambapo akitoa maelezo haya kaimu katibu mkuu wa jumuiya
ya umoja wa vijana ccm Bwn. Shaka Hamdu Shaka Amesema kuwa wao kama
vijana wanaounga mkono juhudi zote zinazotekelezwa na serikali ya awamu
ya tano chini ya mwenyekiti wake Dr.John Joseph Pombe Magufuli wanapenda
kuungana na watanzania wote hususani vijana wote hapa nchini kujitokeza
kwa wingi katika sikukuu ya maadhimisho ya siku ya muungano
Aidha ameendelea kwa kusema kuwa kwa kuwa sherehe hizo
zitafanyika katika mkoa wa Dodoma na hasa ikumbukwe kuwa ndiko kwenye
makao makuu ya nchi pia makao makuu ya chama hivyo vijana wote waliopo
dodoma wajitokeze kwa wingi ili kuweza kuungana na kusherehekea pamoja
kwa siku hiyo ya maadhimisho ya Muungano wa Jamhuri ya Tanzania.
Ambapo ameongeza kuwa wao kama viongozi wa umoja wa
vijana wa ccm(UVCCM) ni wakati wao wa kujivunia na kutembea kifua mbele
na kujisifu kwa ajili ya nchi yao hivyo kwa jambo la maadhimisho ya
sherehe za muungano halina aja ya kujali itikadi za vyama wala ukabila
zaidi wajitokeze kwa wingi mara tu ifikapo siku hiyo ya tarehe
26.04.2017
Post a Comment