RAIS MAGUFULI AIAGIZA TCRA KUYAFUTA MAKAMPUNI YA SIMU AMBAYO HAJAJIUNGA KWENYE SOKO LA HISA
Rais Magufuli ametoa agizo hilo siku ya leo alipokuwa anazindua Mfumo wa Serikali wa Ukusanyaji Kodi Kielektoniki kupitia National Data Center chini ya mfumo uliozinduliwa wa ‘Revenue Collecting System’ (RCS), ili kuwezesha ukusanyaji kodi kwa weledi usiokuwa na mapungufu ya kibinadamu ‘Human Error’
Rais Magufuli amesema serikali ilitoa agizo la makampuni ya simu kujiunga na DSE lakini kampuni ya simu ya Vodacom ndiyo imetii agizo hilo.
Huku akifafanua kuwa TCRA imekuwa ikiyatoza faini ndogo makampuni ambayo hayajajiunga ya kuanzia milioni 300, faini ambayo ni ndogo ukilinganisha na faida yanazozipata, jambao ambalo limepelekea makampuni hayo kulipa tu faini.
Hivyo Rais Magufuli amesema ni bora yafutwe, kwani wanapata mabilioni ya fedha, “Lazima ifike hatua mahali tutoe desicion hata kama zinauma” ameeleza Rais Magufuli.
Na kuongeza kuwa wakijiunga na DSE itazisaidia mamlaka za mapato za Tanzania Bara na Visiwani kukusanya mapato yake.
Post a Comment