Header Ads

header ad

MANISPAA YA ILALA YAFANYA USAFI KATIKA MAENEO KOROFI YA UFUKWENI

Baadhi ya Wakuu wa Idara katika Halmashauri 
ya Manispaa ya Ilala wakifanya usafi.
Viongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kwa kushirikiana na wadau mbalimbali leo wamefanya usafi katika fukwe ya bandari ya Dar es Salaam ambayo imeonekana ni korofi kutokana na uchavu mwingi uliokuwepo katika fukwe hiyo iliyopo Kata ya Kivukoni.

Usafi huo ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuri ambapo kila juma mossi ya mwisho wa mwezi huwa wanafanya usafi hasa katika maeneo ambayo yameonekana Kuwa na uchavi mwingi.

Vijana wa Palepale Jogging wakifanya usafi
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ilala Bernadeter Mwaikambo, amesema kuwa wamekuwa wakifanya usafi huo kila juma mossi ya mwisho wa mwezi kwa ajili ya kuhakikisha maeneo yote ndani ya manispaa hiyo yanakuwa katika hali ya usafi.

Mwaikambo amesema wataendelea kutoa elimu kwa kushirikiana na wenyeviti wa Serikali za mtaa ambao wameonekana kuwa na ushawishi mkubwa kwa wananchi katika kufanikisha suala la kusafisha mazingira linafanikiwa.

Afisa Uhusiano wa Manispaa ya Ilala akiwa katika harakati za kufanya usafi. 
 Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ilala Bernadeter Mwaikambo akifanya usafi.
Amewashukuru watu wote waliojumuika kufanya usafi huku akibaisha kuwa halmashauri imejipanga kuweka mazingira kuwa masafi muda wote.

“Si mpaka kufanya usafi tusubiri mwisho wa mwezi, kwani   mikakati tuliyonayo kwa sasa ni kuendelea kutoa elimu kwa wananchi na kuhakikisha takataka zinazolewa kwa wakati” amesema

Amewataka viongozi wa siasa kuendelea kuhamasisha jamii kwa nguvu kuhusu kufanya usafi katika maeno yote ndani ya manispaa hiyo.

Mkuu wa kitengo cha Idala ya Mazingira Manispaa ya Ilala Abdon Mapunda akifeka majani

Mkuu wa kitengo cha Idala ya Mazingira Manispaa ya Ilala Abdon Mapunda amesema kuwa mazingura kuwa safi ni jambo la muhimu sana kwa binadamu.

Ameesema wameamua kufanya usafi kwenye ufukwe huo kwa sababu maeneo hayo mara nyingi yamekuwa yakisahaulika licha ya kuwa ni makazi kwa baadhi ya watanzania wanaoishi kwenye mazingira magumu.

"Usafi wa mazingira ni jambo muhimu sana kwenye mazingira ya binadamu hivyo ni lazima kufanya usafi kwenye mazingira yanayotuzunguka” amesema  Mapunda.

Mwenyekiti wa Chama Cha Vijana cha Jogging amesema kuwa vijana wanapaswa kujitokeze kwa wingi kufanya usafi kwenye maeneo yao yanayowazunguka na wasione kama wanaonewa na serikali kwani ni wajibu wao kufanya hivyo.

Joseph Amir mkazi wa eneo hilo laufukweni amesema kuwa eneo hilolimeonekana kuwa sugu kwa kuwa na takataka nyingi kwa sababu ya watu kutokuwa na uelewa juu ya kutuza mazingira.

Amesema kuwa ni vema serikali ikatoa adhabu Kali kwa wafanyabiashara wadowadogo wanaolizunguka eneo hilo kwani wao ndio ufanya vitendo hivyo vya kutupa taka ovyo pembezoni mwa bahari.

No comments

Powered by Blogger.