E FM RADIO YATUA MWANZA KWA KISHINDO
Katika azma yake ya kuhakikisha Watanzania wengi wanapata matangazo yake, Kituo cha Utangazaji cha EFM kimetanua matangazo yake kwa kuongeza masafa ya 91.3 fm Mkoani Mwanza huku Uongozi ukibainisha kuwa matarajio ni
kuhakikisha Matangazo hayo yanafika katika mikoa mingine kumi, ikifuatiwa na Mkoa wa Mbeya, Singida, Kilimanjaro, Manyara, Mtwara, Tanga , Kigoma na Dodoma.
Kwa mujibu wa Meneja Mkuu wa EFM Radio Bwana Denis Ssebo, amesema lengo la kuanza na Mkoa wa Mwanza ni baada ya kuangalia idadi ya watu ambao wanapatikana kupitia Kanda ya Ziwa Victoria lakini pia ukubwa wa jiji hilo baada ya jiji la Dar es salaam.
"Lengo la Efm Radio ni kuhakikisha inahabarisha, inaburudisha, kuwezesha pamoja na kuwapa elimu wasikilizaji wake wote katika kila mkoa itakaposikika. Hivyo mikoa mingine ikae mkao wa kula - tutawafuata mlipo…" amesema Denis Ssebo”, akimalizia kwa kusema na EFM NI KWIKWI!
Post a Comment