RC MAKONDA AWATAHADHARISHA WANACHI WALIOPO MAENEO HATALISHI KUTAFUTA SEHEMU SAHIHI
Ikiwa mvua zinaendelea kunyesha katika sehemu mbalimbali zua mkoa wa Dar es salaam,wananchi wa mkoa huo wameomba kuchukua taadhari mapema ya kuhama katika maeneo hayo ikiwa na lengo la kusalimisha usalama wao pindi mvua zinapoendelea kunyesha.
Hayo yamesemwa Leo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda alipokuwa anafanya ziara yake ya kutembelea maeneo mbalimbali yaliyoathiriwa zaidi na mafuriko katika mkoa huo ambapo katika ziara hiyo iliweza kuudhuliwa na viongozi mbalimbali wa serikali, jeshi La zimamoto, Jeshi la polisi pamoja na kamati ya mkoa wa Dar es salaam.
Aidha Makonda amewashauri wananchi ambao nyumba zao zipo sehemu hatarishi kuchukua hatua mapema za kuondoka kwenye maeneo hayo ili kuweza kujikinga na mvua zinazoendele.
"Niwaombe wananchi mliopo sehemu hatarishi kuchukua taadhali ya kuondoka mapema kwenye maeneo hayo ambayo wataalamu wamewaambia kuhama ni heri kuhama na kutafuta sehemu salama ya kuishi" amesema
Pia amewataka wananchi kuacha taratibu za kuchimba mchanga pamoja na kutupa takataka sehemu za madaraja hadi kupelekea kuziba kwa madaraja hayo.
Hatahivyo amesema benki ya dunia imetoa sh Bilioni 1 kwa ajili ya kukarabati daraja la malechela ambalo ujenzi wake utaanza hivi karibuni ambapo ujenzi huo utakuwa chini ya jeshi kusimamia ujenzi huo huo na kuwataka wananchi kutoa ushirikiano.
Wakati huohuo Makonda ameyaagiza maduka yote pamoja na vituo vya daradara vya mkoa huo ndani ya mwezi mmoja kuhakikisha wanaweka vyombo vya kuifadhia uchafu ili kuendeleza usafi na kuondokana na magonjwa ya hapa na pale yanayotokana na uchafu.
"Masikitiko yangu ni kuona huu Mto Ng'ombe watu wanautumia kupakulia vyooo vyao,kutupa takataka, niaibu kubwa kwa mkoa wa Dar es salaam kuwa katika hali ya uchafu na haustahili hata kidogo kua na hali hiyo nataka jiji liwe safi kwa kuweka vifaaa vya kuifadhia takataka ili kila mwananchi akipita aweze kutupa humo " amesema
Makonda amewaomba wananchi wanaoishi karibu na mto Ng'ombe kuwa wasafi ili kuokoa vifo vitokanavyo na ugonjwa wa kipindupindu, ambapo amesema mto huo ulio na km 7.5 umeshatengewa fedha kwa lengo la kuukarabati
Post a Comment