JESHI LA POLISI LAWAJIBU MAWAKILI WA IMMA
Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es Salaam limesema bado linaendelea na uchunguzi kuhusu tukio la mlipuko katika ofisi za kampuni ya Mawakili ya IMMA lililotokea upanga Dar es Salaam na kuwaomba waadhirika wa tukio hilo kuwa watulivu .
Akizungumza na wandisihi wa habari leo jijini Dar es salaam kamishina mwandamizi wa jeshi la polisi ambaye pia anakaimu ukamanda wa polisi kanda maalumu ya Dare s salaam Benedict Kitalika amesema kuwa uchunguzi wa awali uliofanyika umebaini kwamba usiku wa kuamkia tarehe 26 augasti majira kati ya saa 7:00-8:00 watu wasiojulikana utambulisho wao na idadi kamili, walifika katika ofisi za mawakili wa kampuni ya IMMA (IMMA ADVOCATES) wakiwa na magari mawili wakijifanya ni askari na kuwarubuni kisha kuwachukua walinzi wa jengo hilo na kuondoka nao kwenye moja ya gari walilokwenda nalo,ambapo baadaye walinzi hao walikutwa maeneo ya Kawe wakiwa hawajitambui.
Aidha amesema milipuko iliyotokea inaonyesha kuwa ilitengenezwa kienyeji ambapo baada ya watu hao kuondoka ililipuka na kusababisha uhalibifu wa mali na jengo la ofisi hiyo pamoja na majengo ya jirani.
|
Post a Comment