VIJANA KUNUFAIKA NA UJUZI WALIONAO
Serikali
imesema imeshatekeleza mikakati ya kukuza ujuzi wa kusimamia na kuratibu utoaji wa mafunzo ya ujuzi kwa vijana katika sekta mbalimbali ili kuwezesha vijana kuchukua majukumu yao kama viongozi na wazalishaji wakuu hapa nchini.
Akizungumza leo jijini Dar es salaam kwenye mkutano wa kitaifa wa vijana kuhusu afya na maendeleo ambao umewakutanisha wadau mbalimbali Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu ,sera, bunge, kazi, vijana, ajira na wenye ulemavu Jenista Mhagama amesema kati ya sekta ambazo zilizo pewa kipaumbele katika kuwawezesha vijana kuwa viongozi na wazalishalishaji ikiwemo sekta ya ujenzi , sekta ya mafuta na gesi, utalii, kilimo, viwanda vya pamba na bidhaa za ngozi.
Aidha Mhagama amewataka vijana kushirikiana na serikali katika kupiga vita matumizi ya madawa za kulevya ili kuokoa nguvu kazi iliokuwepo kwa ajili ya maendeleo ya taifa ambapo ametoa rai kwa viajana kushiriki katika juhudi zote zinazo fanywa na serikali kuhusiana na maendeleo
Katika hatua nyinge Hatua Nyingine Habari Xtra imetembelea moja kati ya Taasisi ilioshiriki katika mkutano huo Marie stopes inayojishuhulisha na huduma ya ushauri nasaha na uzazi wa mpango ambapo Mshauri nasaha na uzazi wa mpango Dora Kanju kutoka maries topes amesema katika mkutano huo wamejihusisha na utoaji wa elimu kwa vijana ili kujitambua kuhusiana na elimu ya uzazi wa mpango na ushauri nasaha.
Post a Comment