SAMIA AFUNGUA MAONYESHO YA AJIRA KATI YA TANZANIA NA CHINA
Makamu wa rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameipongeza nchi ya China kwa kushirikiana vyema katika uwekezaji na fursa za ajira nchini.
Akizungumza jijini Dar es salaam wakati wa ufunguzi wa awamu ya pili ya maonyesho ya ajira kati ya Tanzania na China mama Samia amesema kuwa nchi ya China ni miongoni mwa nchi zilizowaajiri watanzania mbali mbali katika sekta muhimu hivyo kuna umuhimu kwa nchi hizo kushirikiana katika masula ya ajira.
Naye balozi wa China nchini Tanzania Lee Yon xhi amesema kuwa mpaka sasa China imeshatumia takribani billion 7 katika uwekezaji wake ambapo katika onyesho la mwaka Jana walifanikiwa kuwaajiri watanzania 200.
Naye makamu mkuu wa chuo kikuu cha Dar es salaam (UDSM)Prof RWAKAZA MUKANDALA amesema chuo hicho kinachozalisha wataalamu mbali mbali kitaendelea kushirikiana na wachina katika suala la ajira huku akiwataka waumini wanaohitimu katika chuo hicho kuingia kikamilifu katika soko la ajira.
Post a Comment