KAULI NZITO KUTOA TLS JUU YA SHAMBULIO LA MABOMU KATIKA OFISINI YA MAWAKILI WA IMMA
Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika(TLS), awataka wanachama wote wa TLS nchi nzima kususia kuhudhuria mahakamani kufanya kazi za uwakili na kwenye mabaraza kwa siku mbili (Jummanne na Jumatano) ili kupinga shambulio dhidi ya IMMMA Advocates.
Tundu Lissu amesema tukio hilo sio la bahati mbaya na huenda linahusika na kazi za Mawakili wa IMMMA ambao wanafanya kazi na Kampuni ya Acacia yenye mgogoro na serikali.
Aidha Baraza la uongozi la chama cha mawakili wa Tanganyika (TLS) limelaani shambulio la ofisi ya MAWAKILI WA IMMA lililotokea Jana alfajiri Upanga,Dar es salaam.
amesema Kitendo cha kushambulia ofisi hiyo kwa mabomu inadhihirisha kuwa washambuliaji walikuwa na lengo la kuwatisha mawakili hao na kutishia juu majukumu yao ili kuwatia hofu jambo ambalo halikubaliki.
Aidha LISSU amesema kuwa kitendo hicho kinakiuka Uhuru wa taaluma ya kisheria iliyowekwa na chama cha mawakili duniani.
Hata hivyo ameongeza kuwa mawakili wa kampuni ya EMMA ADVOCATES ndiyo wanayosimamia kesi zake mbali mbali zinazomkabili kupitia wakili FATMA KARUME pamoja na kesi iliyofunguliwa mahakamani ya kampuni ya ACACIA sambamba na kesi iliyofunguliwa mahakama kuu na chama cha wananchi CUF upande wa Maalim Seif jambo ambalo limejenga fikra kwamba huenda ilishambuliwa kwa sababu hiyo.
Ameitaka serikali kupitia vyombo vya ulinzi na usalama kufuatilia tukio hilo kwa haraka ili kupata majibu wa chanzo na aliyeshambulia ofisi hiyo huku akiwataka mawakili wanachama wa TLS kususia kwenda mahakamani na kwenye mabaraza kama mawakili kuanzia siku ya jumanne na jumatano ili kuwaunga mkono mawakili wenzao ambao ofisi yao imeshambuliwa na kusababisha kuharibika,kupotea na kuungua kwa nyaraka jambo ambalo litawasababisha kufanya kazi zao kwa wakati na kuonyesha kuwa hawajafurahishwa na tukio hilo.
Post a Comment