SWIDENI YAMWAGA BILLIONI 435.7 TANZANIA
Serikali ya Sweden imetoa msaada wa jumla ya shil. Billion 435.79 kwa serikali ya Tanzaniawenye lengo la utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo hapa nchini.
Hayo yamebainishwa leo na Katibu wa wizara ya fedha na mipango nchi ni Dotto James wakati wakisaini mikataba mitatu ya makubaliano ya msaada wa kibajeti ukilenga kuimarisha maendeleo mbalimbali nchini ikiwemo miundombinu na kuboresha sekta ya elimu.
Aidha amesema mikataba hiyo itasaidia utekelezaji wa bajeti ya kila mwaka lakini pia kuiwezesha serikali kutekeleza majukumu yake na ukilenga maeneo ya kuboresha uhalisia wa bajeti ili kuweza kutimiza majukumu mbalimbali yaliyokusudiwa kwenye bajeti ya serikali.
Kwa upande wake Mkuu wa ushirikiano wa maendeleo, ubalozi wa Sweden Ulf Kallsting amesema kuwa watahakikisha wanaendeleza ushirikiano kwa serikali ya Tanzania ikiwemo kuboresha sekta ya elimu.
Post a Comment