Header Ads

header ad

ADC YAIJIA JUU CHADEMA


Chama Cha cha Alliance for Democratic Change (ADC), kimekitaka Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Kutoingilia Mgogoro ulikuwepo Ndani ya Chama cha Wananchi CUF.


Akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini hapa  Katibu Mkuu wa Chama Hicho Doyo Hassan amesema kuwa Chadema kuingilia Mgororo wa CUF kunaweza kuhatarisha amani ya nchi Maana Tumeshuhudia Migogoro mingi ya vyama vya siasa lakini hatujaona chama kingine k kikiingilia Mgogoro wa Chama kingine.

Aidha  Doyo ameitaka serikali iviache vyama vya siasa nchini vifanye shughuli zao kwa kumuomba rais Magufuli  kuviachia  vyama vya siasa kufanya mikutano kwani Jambo hilo ni takwa la kisheria

Hatua hiyo imekuja wakati wa kutoa taarifa juu ya Maadhimisho ya kuzaliwa kwa Chama hicho yatakayofanyika Tarehe 22 Agosti Mwaka Huu ambapo chama hicho kitakuwa na ziara kwenye asasi za Kiraia, kuwatembea Wagonjwa, Wafungwa, Vyuo vikuu na Kutembea Nyerere Foundation , na Mwisho kuhitimisha kwenye Ofisi za chama hicho Buguruni Jijini Dar es Salaam.

No comments

Powered by Blogger.