SADAKA ILIYOIBIWA YAKATALIWA, ALIYOIPELEKA KANISANI APIGWA FAINI
Mwanamke huyo ambaye jina lake halijatajwa, anasemekana kumwiba kuku wa jirani hali iliyowafanya Viongozi wa kanisa kulazimika kuingilia kati na baadaye kumpiga faini kwa kitendo hicho
Viongozi wa kanisa na waumini katika kanisa moja la Katikaara, nchini Uganda, wameachwa na mshangao baada ya mwanamke kukamatwa na kuku aliyeibwa na aliyetaka kumtoa kama sadaka kanisani.
Mwanamke huyo ambaye jina lake halijatajwa anasemekana kumwiba kuku huyo kutoka kwa jirani yake Joseph Lutaalo.kwa mujibu wa tovuti moja nchini humo imebaini kuwa, Lutaalo alikuwa amehudhuria ibada katika kanisa hilo iliyoongozwa na kasisi mgeni katika kanisa la Katikaara nchini Uganda
Tukio hilo lilitatiza ibada na waumini kumsikitikia mwanamke huyo. Kulingana na Lutaalo, alikuwa akifuatilia ibada kwa makini alipomwona jirani yake na kuku ambaye alifanana na kuku wake na baadaye kumtambua kuku huyo kuwa wake.. ‘‘Huyu ni kuku wangu; najua wewe ni jirani yangu lakini ni kwa nini ulimwiba kuku wangu na kumleta kanisani?’’ Lutaalo alimuuliza mwanamke huyo. Kabla ya tukio hilo kugeuka kuwa vita, kasisi aliingilia na kuwatawanya 2 hao na baadaye kuamuru viongozi wa kanisa kutatua hali hiyo nje ya kanisa. Hatimaye mwanamke huyo aliyakubali makosa yake na kuomba msamaha kanisani na kuku kurejeshewa mwenyewe.
Post a Comment