SERIKALI KUVIINUA VIWANDA VYA NGUO NCHINI
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa ameambatana na Meneja Mkuu wa Kampuni ya Namera Group of Industries Muhammad Waseem.
Waziri mkuu Kasimu Majiwa amesema serikali
kuvisaidia viwanda vya nguo hapa nchini kupata masoko makubwa
nje ya nchi ikiwa lengo ni kuendeleza dhana ya uchumi wa viwanda.
Akizungumza Jana jijini dar es salaam alipokuwa ametembelea viwanda viwili vilivyo
chini ya kampuni ya Namera Group of
Industries inayomiliki viwandavya Namera na NIDA, Waziri
Mkuu Majaliwa
ameridhishwana uwekezaji uliofanywa na uongozi wa kampuni hiyo huku akisema
serikali
itafanya jitihada mbali mbali kuviunganisha viwanda hivyo namasoko makubwa.
Aidha amesema kuwa juhudi za Tanzania ya viwanda zimefanikiwa kwa asilimia kubwa kwani
wawekezaji wengi na watanzania wanajitahidi kuanzisha viwanda hapa nchini huku
akieleza kuwa kwa Mkoa wa Dar es Salaam kuna viwanda takribani 1845 ambavyo
vimeajiri watanzania wengi.
Waziri Mkuu Kassim
Majaliwa akiwa ameambatana na Meneja Mkuu wa Kampuni ya Namera Group of
Industries Muhammad Waseem.
Waziri Mkuu Kassim
Majaliwa akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Namara Group of
Industries Muhammad Hamza (Mwenye suti ya mistari) na Meneja Mkuu wa kampuni
hiyo Muhammad Waseem (Mwenye suti ya bluu).
Katika hatua nyingine
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliweza kuzungumza na wafanyakazi wa kiwanda cha
NIDA kilichopo maeneo Tabata, ambapo amewasihi wafanyakazi hao kuitumia fursa
hiyo vizuri ya kufanyakazi katika kiwanda hicho cha NIDA kwa kuwa waadilifu na
waaminifu ili wawe mabalozi wema na Tanzania ipate sifa ya kuwa na wafanyakazi
wenye uadilfu jambo ambalo litawavutia wawekezaji wengine.
Kwa upande wa wawakilishi
wa wafanyakazi hao Ahmed Kiumbe alimuomba Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
kushughulikia suala la nyongeza ya mshahara kima cha chini 150,000 ili waweze
kumudu gharama za maisha kwani kiwango wanacholipwa na kampuni hiyo kwasasa
hakitoshi kiwango cha 800,00 mpaka 100,000 jambo linalopelekea wao kuishi
maisha magumu.
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya
Namara Group of Industries Muhammad Hamza (Mwenye suti ya mistari) na
Meneja Mkuu wa kampuni hiyo Muhammad Waseem (Mwenye suti ya bluu)
Post a Comment