TECNO NA JUMIA KUSHIRIKIANA NA TIGO KUUZA BIDHAA MTANDAONI
Katika kuhakisha Watanzania
wanapata Huduma mbalimbali zenye upungufu wa bei nchini Kampuni ya
Jumia Tanzania inayouza bidhaa kwa njia ya mtandao, itashirikiana na kampuni za
simu za Tigo na Tecno kuuza bidhaa zake kwa bei nafuu jambo ambalo litakalowazesha
Wananchi wa vipato mbalimbali kuagiza na kupata bidhaa hizo kwa njia ya
mtandao.
Akizungumza Leo jijini Dar es salaam
na wandishi wa habari Ofisa Uhusiano wa Tecno, Eric Mkomoye, amesema kampuni
yake na Jumia Tanzania wameamua kuungana kutoa huduma popote mteja alipo kwa
njia ya mtandao na Kutakuwa na punguzo kubwa na zawadi mbalimbali kwa
wateja watakaonunua bidhaa hizo katika website yao.
Aidha amesema kuwa Kutakuwa na Jumia
Mobile Week itakayoanza Mei 22 -28 mwaka huu ikiwa maalumu kwa ajili ya
mauzo ya simu na vifaa vyake kutoka makampuni makubwa.
Naye
meneja wa kampuni ya Jumia nchini, Hilda Kinyunyu, amesema kuwa wateja wao wanaweza kuagiza simu kupitia mtandao wa Jumia na kuchagua bidhaa
wanazotaka kisha wanajaza taarifa zao za msingi kama namba za simu na eneo
wanalotaka bidhaa waletewe na watafikishiwa na Malipo yatafanyika baada ya
mteja kupata bidhaa husika na kuridhika nayo.
Kinyunyu amefafanua kuwa kampuni ya Tecno Mobile
itakuwa na duka maalum katika mtandao wa Jumia ambapo simu za kampuni hiyo
ikiwemo simu mpya maarufu ya Tecno Camon CX itapatikana,Pia Tecno Phantom 6, W5
na l9 plus zitapatikana. Mteja atakayweka oda ya simu za Tecno Mobile katika
mtandao wa Jumia atapata zawadi mbalimbali zitakazomfikia pamoja na simu hiyo
Na
James Bayachamo-SalvaNews
Post a Comment