Header Ads

header ad

EAGC KUJADILI UTATUZI WA CHANGAMOTO YA MAZAO YA NAFAKA

 Mkuu mtemdaji wa baraza la Nafaka kwa ukanda wa Afrika mshariki Julius WAMBURA

Baraza la Nafaka la ukanda wa Afrika Mashariki (EAGC) wanaohusika na mambo ya nafaka wameandaa mkutano ambao utajuimisha Wauzaji na wazalishaji wa nafaka ambao utafanyika mwezi Oktoba wenye lengo la kuwakutanisha wazalishaji na wauzaji wa Nafaka na kuzungumzia kuhusu hali na changamoto zinazotokea katika mazao ya Nafaka.



 Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mtendaji mkuu wa Baraza la Nafaka kwa Ukanda wa Afrika Mashariki JULIUS WAMBURA amesema  tangu kutoka kwa uzalishaji ni changamoto zipi zilizopo hasa katika uzalishaji wa nafaka na kujua nini cha kufanya  ili waweze kupata Matokeo tofauti kwa sababu kuna kipindi bei ya Nafaka inakuwa juu na na kipindi kingine bei hushuka kwa kasi sana na mkulima kupata hasara.Hii inaweza kusaidia kutatua matatizo mbalimbali yaliyoko kwenye mazao ya Nafaka.

Aidha amesema   kuwa changamoto iliyoko kwenye zao la soya kwa sasa ni kukosekana kwa mbegu za kutosha kwa baadhi ya wakulima ambazo zinaweza kuzalisha kwa wingi zao hilo.

         Vilevile dhumuni la kuleta mkutano huo nchini Tanzania na kujumuika na nchi mbalimbali ni kuunga mkono Sera ya Muheshimiwa Rais JOHN POMBE MAGUFURI ya Tanzania ya Viwanda.

Na Emanuele Mbatilo Salvahabari

No comments

Powered by Blogger.