Header Ads

header ad

MAARUFU KUSAFIRISHA MADAWA YA KULEVYA CHINA "AKWILAPO''


Wito umetolewa kwa wanafunzi waliopata  nafasi ya kwenda kusoma nchini china kutojihusisha na usafirishaji pamoja na  biashara ya madawa ya kulevya  na tabia zingine zisizofaa .


Wito huo umetolewa  jana jijini Dar es salaam na katibu mkuu wa wizara ya elimu sayansi na teknolojia    Dkt Leonard  Akwilapo wakati akizungumza kwenye hafla fupi ya kuwaaga wanafunzi wapatao 113 waliopata nafasi ya kwenda kusoma nchini china kwa taaluma tofauti tofauti ikwemo ualimu,udaktali ,kilimo, biashara na mambo ya teknolojia.
Aidha Akwilapo amesema kuwa kwa nchi kama china ukikutwa au kushiriki kwa namna yoyote ile kwenye mambo ya madawa ya kulevya adhabu zake ni kubwa ikiwemo adhabu ya kifo  huku akiwasihi kuwa mabalozi wazuri wa nchi ya Tanzania kwa kuwa na maadili yaliyopo nchini.


 Kwa upande wake Mwenyekiti  wa watu waliowahi kusoma china (CAAT),Dkt.Liggy vumilia   amesema kuwa fursa ya vijana wa kitanzania waliyoipata  ya kusoma  china itawapa nafasi ya kujifunza vitu vingi na tofauti  na   vya hapa nchini huku akiwasihi kuiga tabia nzuri zilizopo china kwani vijana wengi wa kitanzania wamekuwa ni watu wakulalamika lakini jambo hilo kwa nchi ya china haipo .


Dkt. Lorna Kasyanju na Josephu Laizer   ni wanafunzi waliyepata nafasi ya kuelekea china kusoma wamewasihisi wanafunzi ambao wamepata nafasi hiyo ya kwenda china kufuata sheria na misingi ya nchi hiyo huku  wakiahidi kwenda kujifunza mambo mbalimbali yakiwemo sheria za mambo ya mafuta na ges ili iwe faida kwa nchi .




Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa watu waliowahi kusoma china (CAAT) Dkt.Liggy vumilia   amesema china imekuwa ikitoa nafasi kila mwaka kwa watanzania kwenda china kusoma masomo mbalimbali.


Na James Bayachamo-Salvanews

No comments

Powered by Blogger.