TAMASHA LA BODA BODA SUPERSTAR LATIKISA DAR.
picha ya Dereva boda boda akishiriki shindano LA kuvuka vizuizi |
Wananchi nao walijitokeza kwa wingi |
Mkurugenzi mkaazi wa IRI Tanzania |
Meneja mkuu wa kampuni ya JP Decaux aliyevaa suti kushoto akisakata rumba baada ya muziki wa singeli kumkosha |
Bodaboda iliyoshindaniwa na kuchukuliwa na mmoja wa madereva boda boda aliyefahamika kama baba Aisha wa kawe |
Msanii wa muziki wa singeli Shoro Mwamba na kundi lake |
Na mwandishi wetu.
Dar es salaa
Maelfu ya wakazi wa jiji la Dar es salaam na viunga vyake pamoja na wakali wa boda boda Jana wamejitokeza kwa wingi kushuhudia onyesho kubwa la madereva wa boda boda katika viwanja vya Tanganyika packes (Kawe) lililoandaliwa na kampuni ya JP Decaux kwa ushkrikiano na shirika la IRI
Awali katika tamasha hilo meneja Mkuu wa kampuni ya JP decaux,SHABAN MAKUGAYA amewaambia wanahabari kuwa lengo la tamasha hilo ni kumtafuta dereva bora wa boda boda katika mkoa wa Dar sambamba na kutoa elimu kwa madereva hao kwa kushirikiana na jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani ili kuwasaidia madereva
hao katika ufanyaji wa kazi zao na kuepuka ajali zinazotokana na ukosefu wa elimu ya usalama barabarani ambapo ambapo madereva wengi walijitokeza kushiriki
Naye mkurugenzi mkaazi wa taasisi ya kimataifa inayojihusisha na masula ya amani (IRI) Bi ROBINA NAMUSISI amesema tamasha hilo pia limetengeneza mahusiano mazuri kwa kuwakutanisha watu wa matabaka mbali mbali pamoja na kuendeleza amani ya Taifa hivyo taasisi yake itaendelea kushirikiana na JP decaux katika matamasha hayo ambayo yatafanyika nchi nzima.
Aidha kwa upande wake diwani wa kata ya kawe,MUTA RWAKATARE amewaambia wanahabari kuwa wakazi wa kata yake wamelipokea tamasha hilo kwa mikono miwili kwani mbali na kutoa elimu kwa madereva boda boda pia limesaidia kuwaunganisha madereva hao sambamba na kusaidia kupunguza matukio ya uhalifu kutokana na madereva hao kujuana na kufanya kazi pamoja kwa amani.
Tamasha hilo ambalo limefanyika kwa Mara ya kwanza jijini Dar pia lilitanguliwa na mechi ya kirafiki kati ya madereva boda boda na askari wa kikosi cha usalama barabarani (Trafiki)ambapo matokeo yaliwapa ushindi Trafiki baada ya kuwatandika madereva hao mabao 2 huku madereva hao wakiambulia goli 1 la kufuata machozi sambamba na kumzawadia piki piki ya King Lion Dereva boda boda aliyeshinda katika kujibu maswali ya masuaka ya usalama barabarani vyema.
Post a Comment