RC MAKONDA AJUMUIKA NA WAFUNGWA DAR KWENYE CHAKULA KATIKA MAADHIMISHO YA UHURU
Kulia ni Mkuu wa mkoa wa dar es salaam Paul Makonda akikabidhi Runinga kwa mkuu wa Magereza
Baadhi ya Viongozi wa Dini waliofika katika kuwafariji wafungwa hao na kuwatia moyo.
Mkoa wa Dar es Salaam umeadhimisha Siku ya Uhuru kwa
Kuwatembelea Wafungwa na Maabusu kisha kupata Chakula cha Pamoja na
kutoa huduma ya Masaada wa Kisheria na Ushauri na Saha kwa Wafungwa na
Mahabusu.
Katika Maadhimisho hayo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe.
PAUL MAKONDA ametoa Msaada wa Runinga za Kisasa 69 (Flat Screen) Touch
zenye ukubwa wa Inch 40 kwa Magereza na Hospital zote za Dar es Salaam
kuwezesha Wafungwa na Wagonjwa kupata haki ya kikatiba ya kupata Habari.
Hii ni Historia kwa Dar es salaam kuwa Mkoa wa kipekee
wenye Runinga Magerezani zinazowawezesha Wafungwa na Mahabusu kupata
Habari na Hotuba za Rais ili kuwapunguzia Msongo wa Mawazo ili wasiwe na
Mawazo ya kujiua ambapo zitagawanywa kwenye Magereza ya Segerea, Keko
na Ukonga.
RC MAKONDA aliongozana na Viongozi wa Dini waliowafariji
Wafungwa na Kuwafanyia Sala na Dua huku Watu wa Ustawi wa Jamii wakitoa
Msaada wa Ushau na Saha kwa Wafungwa.
MAKONDA ambae amepokelewa kwa Furaha kubwa na Wafungwa wa
Gereza hilo amewasihi kutokata Tamaa kwakuwa bado wanayo nafasi ya
kutimiza ndoto zao baada ya kumaliza kifungo ambapo amewahimiza kuwa
Mabalozi Wazuri kwa Jamii.
Ili kupunguza msongamano wa Mahabusu Gerezani RC MAKONDA
amesaidia zaidi ya Mahabusu na Wafungwa 200 wa Gereza la Segerea kupata
Msaada wa Sheria ambao walikuwa hawana uwezo kifedha.
Aidha MAKONDA ametoa Magodoro 100, Vifaa vya Usafi na Sabuni za Kuoga na Kufua kwa Wafungwa na Mahabusu.
Baadhi ya Maabusu na Wafungwa wamemshukuru RC MAKONDA kwa
kuwa kiongozi wa Kwanza na wa pekee aliewatembelea na kupata chakula cha
pamoja, kuwapatia Runinga, kusikiliza changamoto zao na kuwapatia
Wanasheria na watu wa Ustawi wa Jamii kitendo kilichowafariji.
Aidha Wameshukuru pia kitendo cha RC MAKONDA kusikiliza
Changamoto zao na kuzipatia majibu ambapo wamemuahidi kuwa wamebadilika
na watakuwa mabalozi wazuri kuhimiza jamii kuzingatia Sheria.
Post a Comment