HILI HAPA TAMKO LA MCT KUHUSU MWANDISHI ALIYEPOTEA
Kufuatia
kupotea kwa mwandishi wa Gazeti la Mwananchi, Azory Gwanda, Ambaye leo Desemba
9, 2017, ametimiza siku 18 tangu apoteee huko wilayani Kibiti mkoani Pwani,
Baraza la Habari Tanzania (MTL), limetoa tamkoa la kulaani kitendo hicho.
Akizungumza na waandishi wa habari, Katibu mtendaji wa baraza hilo, Kajubi Mukajanga, amesema kuwa wamefanya mahojiano na mke pamoja na watu wa karibu na Azory, ambao kwa maelezo yao inaonekana mwandishi huyo yupo katika mikono salama.
“Ndugu Azory kwa asilimia kubwa kilichomfanya kupotea ni kazi zake, amekuwa akifanya kazi ya kuripoti matukio mbalimbali ya mauaji, tumejiridhisha kwamba ameshikiliwa na watu wasiojulikana kwa sababu ya kazi zake za uandishi, hasa ukizingatia mazingira ya Kibiti yalivyo” amesema Ndugu Mukajanga.

Post a Comment