Header Ads

header ad

PEPSI YAJA NA HILI KWA MSIMU HUU WA SIKUU



                                                               
 Meneja Mfunzo na Uwezeshaji wa Kampuni ya SBC Tanzania Limited Rashid Chenja(wa kati kwenye picha) amezungumza na wanahabari kwenye ukumbi wa habari maelezo jijini Dar es salaam.


bango linaloonyesha shindano hilo la “Jishinde Mamilion
Na Mussa.N.Khalid
Kampuni ya SBC Tanzania Limited imeanzisha shindano kabambe litakalojulikana kwa jina la “Jishinde Mamilion”linalohusu soda aina ya Pepsi,Mirinda Orange,Mirinda Fruity,Mirinda Green Apple,Mountain Dew(300ml)  pamoja na Seven up za ujazo wa mililita 350.

Meneja Mfunzo na Uwezeshaji wa Kampuni ya SBC Tanzania Limited Rashid Chenja amezungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam ambapo amesema lengo la shindano hilo ni kuongeza unywaji wa soda na kuipatia jamii sehemu ya faida ili kuwawezesha kujikomboa kiuchumi.

“Shindano hili litaanzishwa kuanzia tar.4/12/017 mpaka 14/1/2018 katika baadhi ya mikoa nchini ikiwemo Dar es salaam,Pwani,Morogoro,Dodoma,Tanga,Lindi pamoja na Mtwara”amesema Cheja

Meneja Chenja amesema vizibo vya shindano hili vitakuwa na rangi ya silva ambapo kutakuwepo na zawadi za pesa taslimu kiasi cha shilingi 1,000,000/,500,000/-,10,00/-,5000/-,1000/- na soda ya bure.

“Ili mteja ajishindie zawadi anapaswa kununua soda za jamii ya Pepsi kasha abandue ganda ndani ya kizibo akikuta maandishi aidha ya shilingi 1,000,000/-,500,000/-10,000/-1000/-shilingi 5000/-1000/-,na soda ya bure zitapatikana kwa aliyeuza soda,gari ya mauzo au Muuzaji wa Jumla”amesema Maneja Chenja

Kampuni ya SBC Tanzania Limited  ni watengenezaji na wasambazaji wa vinywaji baridi aina ya Pepsi,Mirinda,7up na Mountain Dew .

No comments

Powered by Blogger.