Header Ads

header ad

POLISI YATHIBITISHA KUKAMATWA KWA MWANAFUNZI WA UDSM

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salam limeeleza kuwa ni kweli lilimkamata na kumshikilia mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, anayetuhumiwa kusambaza picha za nyufa zilizopo katika majengo ya hosteli mpya za JPM chuoni hapo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa ameeleza kuwa polisi ilimkamata na kufanya mahojiano na mwanafunzi huyo ili kujua lengo hasa la yeye kusambaza picha hizo pasipo kutoa taarifa kwa wamiliki wa majengo pamoja na wakala wa majengo husika.

“Huyo mwanafunzi alikamatwa na kufikishwa katika kituo cha polisi lakini alihojiwa na kuachiliwa kwa dhamana. Kilichopelekea akamatwe ni ule uzushi awa kuzunguka kwenye kwenye mitando. Sisi tulikuwa tunakitegemea kama angekuwa na taarifa yoyote, wamiliki wa majengo wapo, mkandarasi aliyefanya kazi ile yupo, kwa hiyo mtu ambaye angepaswa kuwa wa kwanza kulalamika angekuwa ni mmiliki wa majengo. Sasa yeye amefikia mahali akarusha, sijui alikuwa na maana gani, hatujaielewa vizuri..,” amesema Kamanda Mambosasa.

Aidha Kamanda Mambosasa alieleza kuwa baada ya kufanya mahojiano na mwanafunzi huyo ili kujua lengo la yeye kufanya kitendo hicho aliachiliwa kwa dhamana.

No comments

Powered by Blogger.