SUMUKUVU YATAJWA KAMA CHANZO CHA KANSA YA INI
Mkurugenzi wa Usalama wa Chakula TFDA Raymond Wigenge akizungumza na wanahabari
Na Mariamu Muhando Dar es salaam
Imekadiriwa kuwa asilimia 30 ya wagonjwa wa kansa ya ini wamepata tatizo hilo kutokana na ulaji wa vya kula vyenye sumu kuvu ikiwemo chakula kinachotoka na zao la mahindi
Hayo yamebainishwa leo Jijini Dar es salaam katika kongamano la udhibiti wa sumu kuvu aina ya aflatoksini katika bara la Afrika PACA kwa lengo la kuzuia ongezeko la sumu kuvu katika vyakula
Akizungumza katika kongamano hilo Mkurugenzi wa Usalama wa Chakula TFDA Raymond Wigengeamsema hivi karibuni kumekuwa na mlikupo wa ugonjwa unaotokana na ulaji wa mahindi yenye sumu kuvu katika nchi za Kenya na Tanzania ambapo zaidi ya asilimia 20 ya watu walioathirika walifariki
Hata hivyo Wigengeamebainisha malengo mbalimbali ya kongamano hilo ikiwemo kuongeza uelewa wa tatizo la sumu kuvu katika sekta ya afya, kilimo na biashara
Kwa upande wake Mshauri wa masuala ya sumu kuvu umoja wa Afrika PACA PROF Martin Kimanyaamsema ziko mbinu mbalimbali ambazo zitumika katika kuhakikisha kuwa tatizo la sumu kuvu linakabiliwa ikiwemo suala la uelewa na elimu juu ya tatizo hilo kwa wananchi.
Post a Comment