Header Ads

header ad

WALIOBOMOLEWA BUGURUNI WALIPWE"NYANDUGA"


Tume ya haki za binadamu na utawala bora imesema kuwa zoezi la ubomoaji wa nyumba 72 za wakazi wa kata ya kwamnyamani Buguruni jijini Dar es salaam lilikua  na ukiukwaji wa sheria hivyo imezitaka mamlaka zizohusika na zoezi hilo kuwalipa fidia waathirika waliobomolewa nyumba zao.

Akizungumza na wanahabari wakati wa kutoa mapendekezo hayo,Mwenyekiti wa Tume hiyo Bahame Nyandugaamesema kuwa hatua hiyo imekuja baada ya  kamati ya waathirika wa kuvunjiwa nyumba kutoka kata ya Kwamnyamani Buguruni Jijini Dar es salaam kuwasilisha malalamiko kwa tume hiyo baada ya nyumba zao kuvunjwa na kukosa sehemu yakuishi.

Mapema mwaka huu Kampuni hodhi ya rasilimari za reli(Rahco) ilisaidiana na kampuni ya Hepautwa Investment and General Broker Ltd  pamoja na jeshi la Polisi  kubomoa nyumba 72 ambazo zilidaiwa zipo ndani ya mita 30 kutoka  kwenye reli kwa mujibu wa sheria,



Baada ya kutolewa tamko hilo Mwanasheria wa kampuni hodhi ya rasilimali za reli(Rahco) Pamela Swaiamesema kuwa wamepokea maamuzi yaliyotolewa na tume hiyo nakwamba wanaenda kuyafanyia kazi.


Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya waathirika waliyobomolewa nyumba zao Msafiri Mihamed Bonamali amesema wamefurahishwa na uwamuzi wa tume hiyo kwamadai kuwa umetenda haki na aikuonyesha upendeleo.



Tume ya haki za binadamu na utawala bora imetoa siku tisini kwa mamlaka zilizohusika kubomoa nyumba hizo kuhakikisha zimeyatekeleza mapendekezo ya tume ambayo yatawasilishwa kwa mamlaka husika chini ya kifungu namba 28 ibara ndogo ya 1 na ya 2 ya sheria ya tume sura391 ya sheria za Tanzania toleo la 2002.

No comments

Powered by Blogger.