MSTAHIKI Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya
Mwita ameondoka Nchini usiku wa kuamkia leo kuelekea Nchini Ujerumani kuhudhuria
mkutano wa mameya wote Duniani unaofanyika nchini humo.
Meya Mwita ameondoka Nchini hapa akiwa
ameambatana na Mkugenzi wa jiji Spora Liana ,Afisa Mipango miji wa jiji, ambapo
watakuwa nchini humo kwa muda wa siku nane na kurejea jijini hapa Novemba 15.
Meya Mwita amehudhuria mkutano huo wenye lengo
la kujadili suala la mabadiliko ya tabia ya nchi hususani katika kukabiliana na
janga la mafuriko kwenye maeneo ambayo hukumbwa na changamoto hiyo.
Aidha katika mkutano huo, Meya Mwita atatumia
nafasi yake kushawishi Umoja wa Mataifa, Mameya sambamba na Taasisi zinazo
husika na mabadiliko ya Tabia ya Nchi kusaidia changamoto za mafuriko ambazo
zimekuwa zikilikabili jiji la Dar es Salaam.
Meya Mwita alisema kuwa kupitia mkutano huo, wakazi
wa jiji la Dar es Salaam wategemee mabadiliko makubwa katika suala zima la
utatuaji wa changamoto ya mafuriko.
Hata hivyo baada ya kumaliza kwa mkutano huo
atakunata na kufanya mazungumzo na Meya wa jiji la Hamburg ambapo awali
walikuwa na makubaliano ya kuboresha miundombinu ya kuhifadhia takataka katika
halmashauri ya Kinondoni (Dampo).
Post a Comment