MWIGULU AWASHANGAA WAPINZANI KWA KUWEKA WAGOMBEA KATIKA UCHAGUZI MDOGO WA MADIWANI
Waziri wa Mambo ya Ndani na Mjumbe wa halmashauri kuu ya chama cha
mapinduzi CCM Mwigulu Nchemba amewashangaa vyama vya upinzani kwa kuweka
wagombea katika uchaguzi mdogo wa madiwani nchini kwani kwasasa ilani
inayofanya kazi ni ya CCM sasa hao wagombea upinzani wanaenda
kutekeleza ilani gani.
Hayo ameyasema akiwa katika kata ya siuyu jimbo la singida mashariki wilaya ya Ikungi alipokuwa akifungua kampeni za mgombea Udiwani kupitia tiketi ya CCM baada ya diwani Gerald Mahami aliyekuwepo wa CHADEMA kuvuliwa uongozi kutokana na kutoshiriki vikao vya baraza la madiwani la halmashauri ya ikungi alipoongozana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida na mbunge wa viti maalum Matha Mlata na mbunge wa singida magharibi Elibariki Kingu.
Waziri Mwigulu amesema uchaguzi wa mwaka 2015 kila mtu alileta mgombea wake akiamini atashinda na baadae mgombea wa CCM Rais Dr Johm Magufuli alishinda na ilani ya CCM ndio inayotekelezwa hivyo haoni haja ya wapimzani kusimamisha mgombea kwani kwasasa ilani ya CCm ndio inayofanya kazi sasa hao wagombea watafanyia kazi ilani ipi.
Waziri Mwigulu amesema kuwa watu kuwa na vyama vingine sikosa na wala kuwa na kadi ya chama kingine si lazima upigie chama chako bali upige kura kwa diwani ambaye ilani yake ndio inatekelezwa kwa wakati huo ambapo atakuletea maendeleo.
Mgombea Udiwani wa kata ya Siuyu Mgonto Juma RamadhaniI amewaomba wananchi kumchagua iliaende kuwawakilisha katika baraza la madiwani katika kutatua tatizo la maji ambalo lipo kwa mda mrefu na tatizo la barabara ambayo ni mbovu sana japo kuwa wana mbunge ambaye hawatetei kabisa katika kupata barabara ya kiwango cha lami ndani jimbo lao na kuwaahidi wananchi kuwa ndani ya kipindi hiki cha miaka mitatu iliyobaki atafanikisha asilimia kubwa ya matatizo yanayowakabili wananchi wake ameyatatua kwa kuongea na viongozi wa juu kuyamaliza kwani kwake ni rahisi sababu wanakutakana katika chama.
Mbunge wa singida magharibi Elibariki Kingu ambaye ni mbunge jimbo jirani na singida mashariki amewahaidi wananchi wa kata ya siuyu kuwa atakuwa mlezi wa kata hiyo na wakifanikisha kumpitisha diwani wa CCM vicoba ya kina mama atawachangia milioni 15 huku hakiadi ofisi ya chama kuwapa milion moja endapo mgombea wao atashinda na kuhusu swala la maji atamleta waziri wa maji ili kuja kutatua tatizo hilo.
Uchaguzi katika kata ya Siuyi unafanyika baada ya Diwani Gerald Mahami Ialiyekuwepo kutoka upinzani (CHADEMA) kuvuliwa udiwani baada ya kushindwa kuhudhulia vikao vya baraza la madiwani.

Post a Comment