Header Ads

header ad

WACHIMBAJI WADOGO WAANDALIWA KIBANO

 

Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga imepitisha mapendekezo ya sheria ndogo ya kuwabana wachimbaji wadogo wa madini kulipa ada na ushuru, hatua itakayosaidia kuongeza ukusanyaji mapato na kufanya shughuli za maendeleo.

Mapendekezo ya vifungu vya sheria ya ada na ushuru ya mwaka 2017 ambavyo ni vipya vimepitishwa juzi na baraza la madiwani wa halmashauri hiyo, inataka kila mtambo wa uchenjuaji kutozwa Sh7 milioni kwa mwaka.

Akizungumza kwenye kikao hicho mwenyekiti wa Halmashauri ya Shinyanga, Ngassa Mboje alisema hatua hiyo inalenga kuongeza mapato kupitia vyanzo vyake vilivyopo ikiwamo uchimbaji mdogo wa madini ambao ulianza wakati sheria ikiwa imeshatungwa.

Katika sheria hiyo mpya inaelekeza malundo ya udongo wa dhahabu kulipiwa asilimia 10 na mawe yenye dhahabu yatalipiwa asilimia 25, huku kila mtambo wa uchenjuaji ukitozwa Sh7 milioni kwa mwaka. “Kampuni au mwekezaji atakayekuja kutandaza mabomba ya maji, mafuta au gesi atatozwa ushuru kwa mujibu wa sheria ndogo, hii inatokana na wakati akifanya shughuli hizo uhalibifu wa miundombinu ya barabara utatokea na gharama zitabaki kwa halmashauri,” alisema.

Akiwatetea wachimbaji, diwani wa Mwakitolyo ambako kuna mgodi wa wachimbaji wadogo, Augustine Limbe alisema wachimbaji wadogo wanatumia gharama kubwa kulipa ushuru wa kijiji, hivyo kuwawekea tozo nyingi kuna wapa mzigo kwani wapo tayari kulipia Sh50,000 kwa mwaka.

Naye mwanasheria wa halmashauri hiyo, Musa Mpogole alisema sheria mpya zilizopendekezwa mashimo yakutolea dhahabu, mwalo wa kuchenjulia, kibali cha magari yanayofanya biashara mgodini na mitambo ya kusaga mawe vitattozwa Sh20,000
kwa mwezi

No comments

Powered by Blogger.