HOSPITAL YA AGA KHAN YALETA HAUWENI YA SARATANI YA MATITI.
Hospitali ya Aga Khan iliyopo jijiji Dar es Salaam imefanikiwa kuanza kutoa huduma ya matibabu ya kufanya upasuaji wa kitaalamu wa kutengeneza matiti ya kinamama ambao wameathirika na ugonjwa saratani.
Matiti hayo yanatengenezwa kitaalamu kwa kufanyiwa upasuaji muhusika ili kurudisha matiti yake ingawa haitarudi katika hali yake ya kawaida kama ilivyokuwa awali kabla ya kupata ugonjwa wa saratani ya matiti.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Daktari Bigwa wa Upasuaji kutoka hospital ya Aga Khan Dk. Aidan Njau, amesema kuwa hatua hiyo itawasaidia wakina mama ambao watakuwa wameathirika na saratani ya matiti.
Daktari Bigwa wa Upasuaji kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dk. Edwin Malima katikati akizungumza na waandisshi wa habari. |
Amesema kuwa hii ni mara ya kwanza kufanyika, hivyo italeta hauweni kwa wagonjwa kutokana waliokuwa wanajisikia vibaya baada ya kupata ugonjwa wa saratani ya matiti.
“Tutaweza kurudisha matiti ya kinamama ambayo yalitolewa kutokana na saratani, hivyo itakuwa faraja kwao kwani watakuwa katika hali ya kawaida kimuonekano kama ilivyokuwa awali kabla ya ugonjwa” amesema Dk Njau.
Hata hivyo amefafanua kuwa elimu hiyo ya kitaalamu ya kufanya upasuaji wa kurudisha matiti ya kinamama ameipata nchini Marekani baada ya kwenda kusoma huko (Scholar ship).
Naye Daktari Bigwa wa Upasuaji kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dk. Edwin Malima zoezi hili linapaswa kuugwa mkono na watanzania wote.
Amesema kutokana na hatua hiyo wameamua kuwapeleka wanafunzi wawili wa Chuo Cha Muhimbili (MUHAS) katika hospitali ya Aga Khan kwa ajili ya kupata elimu ya kufanya upasuaji wa kutengeneza matiti ya kinamama.
“Wamekuja kujifunza jinsi ya kufanya upasuaji wa kurudisha matiti ambayo yalivunwa kutokana na ugonjwa wa saratani” amesema Dk. Malima.
Post a Comment