PICHA YA MIAKA 50 ILIYOPITA KUONEKANA NCHINI
Mkurugenzi
Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Pro. Audax Mabula aliyepo katikati, aliye
upande wa kushoto ni mpiga picha mkongwe kutoka Nchini Denmark Jester
kirknaes.
Makumbusho
ya taifa Tanzania,kwa kushirikiana na bwana Jesper Kirknaes kutoka
Dernmark ,kwa udhamini wa ubalozi wa denmark nchini imeandaa onyesho la
picha liitwalo"Karibu Tanzania"Kuuhusu kazi mbalimbali na maisha ya
watanzania miaka 50 iliyopita.
Akizungumza
na waandishi wa habari mkurugenzi mkuu wa makumbusho ya Taifa
Prof:Audax Mabula,Amesema onyesho hili litafunguliwa rasmi na mheshimiwa
balozi wa denmark nchini Einah .H.Jensen tarehe 16/11/2017 saa saba
7:00 mchana katika makumbusho ya taifa dar es salaam,Ambapo amesema
mabalozi,viongozi mbalimbali na wananchi wanatarajiwa kuudhuria ufunguzi
huo.
Amesema,Onyesho
hili litahusisha maonyesho ya vifaa na picha mbalimbali zinazohusu
maisha na kazi zilizokuwa zinafanywa an watanzania,na kufafanua kuwa nia
ya kuweka onyesho hili ni kuonyesha uhalisia wa kazi na maisha ya
watanzania miaka 50 iliyopita halia ambayo ingekuwa ni vigumu kuelezea
kwa maneno
Sanjari
na ,picha vionyeshwa halisi vitakuwepo ili kutoa fursa kwa watu kuona
jinsi ilivyokuwa vinatengenezwa hatua kwa hatua mpaka kupata kifaa
husika,picha hizo,zilipigwa mwanzoni mwa mwaka 1968 hadi mwaka
1977,amesema kuwa picha hizi zinaumuhimu mkubwa kihistoria na
kiutamaduni kutokana na mabadiliko ambayo tunayoyaona sasa katka jamii
zetu.
"Kwa mfano kila kabila lilikuwa na aina yao ya nyumba na walijitegemea vyombo vyao vya nyumbani kama vyungu,vikapu,nakadharika".
Hata
hivyo,amesema katika wakati huu ambapo Tanzania , jnlekea kuwa na
uchumi wa viwanda onyesho hili linatoa funzo kubwa kutokan na kwamba
watanzania wenzetu ambao waliweza kuendesha maisha yao kujtengenezea
vitu walivyovihitaji wenyewe katika ulimwengu wa sayansi na teknologia
bado watanzania wanaweza kufanya mambo makubwa kuliko waliofanya miaka
mingi iliyopita.
Pamoja
na hayo,prof:Mabula amesema kuwa uwepo wa onyesho hili katika
makumbusho ya taifa n sehemu sahihina amewataka watu kwenda kwa wingi
kujionea wapi jamii ilikotoka na wapi inakokwenda.
Post a Comment