MADAKTARI 300 KUTOKA CHINA KUWATIBU WAKAZI WA DAR
Akizungumza Na Vyombo Vya Habari Hivi Leo Mkuu Wa Mkoa Wa Dar Es Salaam Paul Makonda Amesema Kuwa Kufuatia Juhudi Zilizoonyeshwa Na Mkoa Hasa Za Upimaji Wa Afya Bure Zoez Ambalo Liliendeshwa Kwa Takriban Siku Saba Huku Mwamko Ukiwa Mkubwa Ndio Kilichopelekea Aliekua Balozi Wa China Nchini Tanzania Kuahid Kusaidiana Na Ofisi Ya Mkoa Katika Kuongeza Nguvu Zaidi Za Madaktari Bigwa Toka China Ili Waje Watoe Huduma Hiyo Ya Vipimo Pamoja Na Matibabu Bure Kwa Muda Wa Siku Saba Kuanzia Tarehe 20.11.2017 mara baada ya meli hiyo kutia nanga tarehe 19 ya mwezi huo.
Ambapo Rc Makonda ameongeza kwa kusema kuwa hiyo ni fursa nyingine kwa wananchi na wakazi wote wa Dar es salaam kujitokeza kwa wingi ili waweze kupewa huduma hiyo hasa kwa wale wenye magonjwa kama kisukari,figo moyo,presha nk. wote kwa pamoja kufika kwa wingi katika eneo ambalo limetengwa maalumu kwa ajili ya uchunguzi na matibabu hayo ambayo yatafanyika ndani ya meli katika eneo la bandarin jijini hapo.
Akitaja idadi ya wagonjwa kwa siku ambao watatibiwa na kupewa vipimo Rc Makonda amesema wagonjwa wapatao 600 kwa kila siku ndio watakao kuwa wakihudumiwa,sambamba na hayo wagonjwa wote ambao watapimwa na kugundulika na magonjwa basi watapewa huduma hapohapo kwenye eneo la kutolea huduma lililopo ndani ya meli hiyo,
Post a Comment