CUF YAMJIBU MBOWE
Chama cha wananchi -Cuf kimesikitishwa na kauli za maudhi na zenyekuleta chokochoko zilizotolewa na Mwenyekiti wa Chadema Ndugu Freeman Mbowe huko Mtwara.
Kati hali inayoonyesha kua Chadema imekosa agenda kwenye Chaguzi ndogo zinazorejewa kwenye Kata 43, imeamua kuanzisha mashambulizi yasiokua na tija kwa Wapiga Kura wa Kata husika wala Chadema yenyewe kama Chama .
Kuacha kueleza Sera za Chama chao kwa Wapiga Kura ili iwe chachu ya kuchaguliwa kwa Wagombea wao, Freeman amegeuza Majukwaa hayo kua uwanja wa mashambulizi binafsi dhidi ya Profesa Lipumba.
CUF-Chama cha Wanachi sio tu tumeshangazwa lakini pia tunajiuliza kwani Prof Ibrahim Lipumba ni mgombea wa Kata ipi kati ya hizi zinazorejea Uchaguzi?
Hivi Mbowe anaweza kuhoji Uprofesa wa Lipumba kwani hajui sehemu za kupata majibu yake?
Kama hajui basi tunamsaidia na aende UDSM au William College Marekani atapata majibu ya swali lake kama yeye hawezi kufika maeneo hayo basi watafute wenye kuweza kufika maeneo hayo.
CUF-Chama cha Wanna hi hakina cha kuhoji wala kuuliza Mbowe ni Mwenyekiti wa aina gani kwakua kinamtambua vyema na hasa kupitia wakati wa uhai wa Club Bilcanas kwa hivyo mtazamo na fikra hasi sio tu dhidi ya Prof Lipumba lakini pia hata kwa Siasa za Nchi yetu ni matunda ya Club Bilcanas.
Mhe Mbowe anafahamu kwamba yeye na Prof Lipumba ni sawa na Mlima Kilimanjaro na Kichuguu kuhusu Elimu hivyo kuhoji Elimu ya Prof Lipumba ni kichekesho sana.
Mhe Mbowe anatambua sababu ya Prof Lipumba na Dkt Slaa kutoshiriki Kampeni za kumnadi Lowassa ni kutokana na Mgombea huyo kukosa sifa za Uadilifu na tuhuma mbalimbali za Ufisadi zilizoelezwa hata na yeye mwenyewe Mbowe.
Mbowe sio mkweli hapo Mtwara mjini licha ya kuwepo kwa mashirikiano ya UKAWA chadema iliweka mgombea na mgombea wetu alishinda wwagombea wote wa CDM,CCM,ACT-WAZALENDO,na NCCR-MAGEUZI.
Lakini katika hotuba yake amedai eti!!
Mtwara mjini hawakuweka mgombea siasa za Utapeli zimepitwa na wakati ni vema tukajikita kueleza kero za watu na namna ya kuzitatua.
Tunapenda kumfahamisha Mbowe na wenzake hatuhitaji chokochoko kwanzia sasa kitendo chochote cha kumkashifu Mwenyekiti wetu hakitavumilika. Tutajibu kwa mifano hai itayoleta tija kwa Jamii kwani kila jambo litavuliwa nguo .
Imetolewa
Abdul Kambaya Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma
13/11/2017
Post a Comment