HUU HAPA WITO KUTOKA BAKWATA KWA WAISLAM
Jumuiya ya Vijana wa Kiislamu BAKWATA
Taifa, inampongeza Muft wa Tanzania Sheikh Abuubakar Zubery bin Ally
kwa kazi kubwa ya kuleta maendeleo katika uislamu kwa miaka miwili
aliyohudumu katika cheo hicho tangu tarehe 10 Septemba 2015.
Akizungumza Jijini Dar es Salaam katika
eneo la Masjd Ghadir Katibu wa Jumuiya ya Vijana BAKWATA Sheikh Othman
Zuberi amesema tangu alipochaguliwa Muft Abubakar mwaka 2015 ameweza
kufanya mambo mbalimbali baada ya kutoa maelekezo kwa viongozi wa dini
ikiwemo kudumisha amani, kuunganisha jamii, kuleta maendeleo,
ushirikiano mzuri wa Baraza na Mashirika ya Dini ya ndani na nje ya
nchi, kuamrisha mema na kukataza maovu, uboreshaji wa elimu ya dini na
secula, kusisitiza kujitambua, mahusiano mazuri kati ya Baraza na
viongozi wa nchi, kukataza kufanya kazi kwa mazoea, na sensa kwa
maendeleo ya waislamu ambapo ameagiza kupatikana kwa takwimu sahihi kwa
waislamu kupitia misikiti mbalimbali hapa nchini.
Katibu huyo amewatoa hofu waislamu
kuhusu suala la sensa kwa waislamu na kuwaambia wasiwe na hofu kwani
hata katika kitabu kitukufu cha Qur-an kimewataka waislamu kufanya mambo
kwa mahesabu hivyo wamuunge mkono Muft Abubakar kwa kufanya hivyo.
Na kuwapongeza makatibu wa mikoa na Wilaya mbalimbali walioanza zoezi la sensa kwani sensa ni kwaajili ya maendeleo ya waislamu.
Katibu huyo amewataka viongozi na Taasisi mbalimbali za dini kumuunga mkono Muft Abubakar kwa maendeleo ya waislamu.
Post a Comment