MAAMUZI YA MPINA BAADA YA KUSHUHUDIA MIZOGA YA NG'OMBE 692
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina
ameamuru ng'ombe waliobaki hai kati ya 692 waliokufa katika Pori la
Akiba la Rukwa/Lwafi, waliokuwa wameshikiliwa warudishiwe kwa wamiliki
wa mifugo hiyo.
Akiwa katika ziara yake Mh. Mpina
amelazimika kutoa maamuzi hayo baada ya kukuta mizoga 692 ya ng’ombe
ikiwa imetapakaa katika Pori hilo ambapo imedaiwa kwamba ng'ombe hao
walikufa kwa kukosa mahitaji muhimu.
Waziri Mpina ameshangazwa kuona mizoga
mingi kiasi hicho huku mifugo hai ikiishi zizi moja na iliyokufa, huku
kukiwa na harufu mbaya
Imeelezwa kwamba mazingira hayo
yamechangia kasi ya maambukizi ya magonjwa nyemelezi kuwa kubwa zaidi na
kupelekea ongezeko la vifo kwa mifugo hiyo.
Hata hivyo baada ya kushudia Mizoga
hiyo, Mh. Mpina amepokea taarifa ya Mkoa, Wahifadhi, Chama cha Wafugaji
na wamiliki wa mifugo hiyo na kupitia nyaraka mbalimbali, ilibainika
kuwa Mahakama Kuu, Kanda ya Sumbawanga, ilitoa amri ya ng’ombe hao
kukabidhiwa kwa wenyewe tangu Julai 27, mwaka jana.
Mifugo hiyo ilikuwa imehifadhiwa katika hifadhi hiyo tangu mwezi machi mwaka jana.
Post a Comment