Header Ads

header ad

SERIKALI YATAKIWA KUWEKA MIKAKATI MADHUBUTI KATIKA MALEZI YA WATOTO



 
 
Serikali kwa kushirikiana Taasisi wanapaswa kwa na mikakati mbalimbali ya kulinda mtoto kabla ya kuzaliwa ili kutenda maendeleo katika nyanja zote.

Hayo yamebainisha katika Maadhimio ya Mkutano wa Kimataifa wa kujadili malezi na makuzi ya watoto uliomalizika leo jijini Dar es Salaam ambapo wasomo, Watafiti kutoka nchi mbalimbali walishiriki.

Mkutano huo uliofanyika kwa muda wa siku tatui umeandaliwa na Taasisi ya Chuo Kikuu cha Aga Khan, Taasisi ya Maendeleo ya Binadamu (IHD) kwa kushirikiana na The Conrad Hilton Foundation.
 Akizungumza na waandishi wa Habari Mkurugenzi wa Aga Khan Foundation, Profesa Kofi Marfo, amesema kuwa ni wajibu wa maendeleo ya watoto hutegemea kila mtu kuanzia wazazi, jamii hadi Taifa.

“Kila mtu ana jukumu kujenga mazingira salama kwa watoto wetu kucheza, maji salama, lishe bora, vituo vya afya na hospitali hivyo ni muhimu kuwekeza katika sera nzuri, huduma na mipango ambayo itaimarisha misingi ya maendeleo ya binadamu,” amesema Profesa Marfo. 


Amewataka wadau wote kutafuta mabadiliko ambayo yanafanya uwekezaji wa muda mrefu katika sera, huduma za mipango ambayo itaimarisha misingi ya maendeleo ya binadamu.


“Maisha yetu ya baadaye katika jamii inategemea mabega ya watoto wetu ikiwa tunashindwa kujenga misingi imara ya baadaye katika mafanikio kwa watoto wetu, hakuna wakati ujao wa kuzungumza” amesema Profesa Marfo.


Hata hivyo inaelezwa kuwa zaidi ya watoto milioni 250 ulimwenguni kushindwa kupata uwezo wa kupata maendeleo kutokana na umaskini, utapiamlo katika miaka ya mwanzo ya kuishi.

No comments

Powered by Blogger.