TIOB YAJA NA UTARATIBU HUU KWA WANACHAMA WAKE
Taasisi inayosimami taaluma ya Kibenki ya TIOB imeanzisha kampeni ya kuwatafuta mabalozi wa taasisi hiyo(TIOB AMBASSADOR CAMPAIN) ambao watasaidia kuwafikia wanachama wa taasisi hiyo kwa urahisi.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Msajili wa Taasisis hiyo MH. SAADI BANZI amesema mnamo tarehe 31 Julai 2017 TIOB ilizindua rasmi Dodoso kwa njia ya Mtandao kwa ajili ya kuboresha shughuli za Taasisi.
Vilevile amesema Balozi wa TIOB ni mwanachama ambaye ameweza kutoa Taarifa juu ya uwepo wa Dodozo kwenye Tovuti ya Taasisi kwa wanachama wenzake na hatimaye kuwawezesha wanachama hao kujaza Dodoso hilo na kuliwasilisha kwa Taasisi na tovuti hiyo ni www.tiob.or.tz.
Na pia ameeleza kuwa zawadi zimeandaliwa kwa mabalozi watano (5) washindi watakofanikisha wanachama wengi kujaza Dodoso na zawadi hizo zitakuwa za kugharamia malipo kwa ajili ya mitihani na vitabu.
Namna ya kushiriki ni kujaza fomu za kushiriki kama balozi na kuweka taarifa zako zote na wale ambao uliowapa taarifa juu ya uwepo wa Dodoso ukitaja namba za usajili na kuziwakilisha kwao kwa ajili ya mchanganuo ili kupata washindi na mwisho wa zoezi hili ni tarehe 30 septemba 2017.
Na Emanuel Mbatilo -Salvahabari
Post a Comment