AGIZO LA SERIKALI JUU YA MALEZI KWA WATOTO
Akifungua mkutano wa Watafiti,Wasomi, na watunga sera waliyokutana leo jijini Dar es salaa katika warsha ya siku tatu iliyoandaliwa na taasisi ya maendeleo ya Kibinadamu ya Chuo kikuu cha Aga khani (IHD) Naibu Katibu Mkuu wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Ave maria Semakafu ambaye alikuwa amemuwakilisha waziri wa Wizara hiyo Prof.Joyce Ndalichako, amesema kuwa kumuendeleza mtoto kimakuzi siyo jukumu la serikali pekee bali ni ushirikiano wa wadau wote .
Aidha Semakafu amesema serikali itaendelea kuboresha na kusimamia sera ya mtoto ili kuwezesha watoto kupata huduma muhimu ikiwemo elimu na lishe bora pamoja na masuala ya kiafya kwa ujumla kwani mtoto ni taifa la kesho.
Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya maendeleo ya Elimu kutoka Chuo Kikuu cha Aghakani(AKU) Prf.Joe Lugalaamebainisha kuwa ili Tanzania na Nchi zingine ziweze kufanikisha kuwekeza katika makuzi bora ya mtoto ,ni muhimu kupiga vita umasikini.
Kwa upande wao baadhi ya wazazi kutoka jijini mwanza wameiambia Salvahabari kuwa Bado kwa hapa Tanzania kumekuwepo na changamoto nyingi za kimalezi ikwemo ukatiri dhidi ya watoto, kukatishwa kwa masomo hata kipato kutotosha kumsomesha mtoto
Awali akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano huo Mkurugenzi wa taasisis ya Maendeleo ya Kibinadamu ya Chuo Kikuu cha Aga khani (IHD ).Prof Kofi Marfoamesema kuwa mkutano huo umewakutanisha washiriki kutoka nchi zaidi ya 30 kwa ajili ya kujadili mambo mbalimbali yanayohusu haki za mtoto ikiwa ni pamoja na huduma bora za afya,elimu ,usalama wa watoto,maji salama,ambapo jitihada hizo ni jukumu la mtu,wazazi,familia,jamii na taifa kwa ujumla.
Mkutano huo wa pili wa kimataifa ambao shabaha yake kubwa ni kujadiliana namana ya kuweka mikakati juu ya maendeleo ya makuzi ya Mtoto,Umeitishwa na Taasisi ya Maendeleo ya Kibinadamu ya Chuo kikuu cha Agakhani(IHD) kwa kushirikiana na shirika laConrad N.Hilton,ambapo umetanguliwa na ujumbe wa“Maendeleo ya Mapema ya Watoto katika nyakati zisizo uhakika”
Post a Comment