HAYA HAPA MAUZO YA SOKO LA HISA DAR ES SALAAM KWA WIKI HII
Thamani ya mauzo ya hisa katika soko la hisa la dare s salaam (DSE) imepanda kutoka Shilingi Billioni 3 ya wiki iliyoishia 3 Novemba 2017 hadi Shilingi Bilioni 86 kwa wiki iliyoishia 10Novemba 2017 Huku hisa zilizouzwa na kununuliwa imepanda kutoka hisa Mil 3.5 ya wiki iliyoishia 3 Novemba 2017 hadi hisa Mil 9 ya wiki iliyoishia 10 Novemba 2017.
Mery Kinabo ni afisa mwandamizi kutoka Soko la hisa dar es ameiambia Times fm kuwa Ongezeko hilo kubwa la mara moja limetokana na ununuzi wa hisa za TBL kwa kampuni tanzu ya SABMiller huku
Kampuni zilizoongoza katika mauzo ya hisa ni TBL99%,CRDB, 0.56% naVODA.0.01%
Kampuni zilizoongoza katika mauzo ya hisa ni TBL99%,CRDB, 0.56% naVODA.0.01%
Aidha amesema kuwa Ukubwa wa mtaji wa kampuni zote zilizoorodheshwa katika soko umepanda kwa Shilingi Bilioni 525 kutoka Shilingi Trilioni 20.2 wiki iliyopita hadi Shilingi Trilioni 20.8 wiki iliyoishia tarehe 10 Novemba 2017. Ongezeko hilo limetokana na kupanda kwa bei za hisa za KCB (15%), NMG (10%), KA (9%) na TBL (1%).
Mauzo haya yalitokana na hatifungani saba (7) za serikali zenye jumla ya thamani ya Shilingi Bilioni 12.5 kwa jumla ya gharama ya Shilingi Bilioni 11.2
Post a Comment