MCT KULA SAHANI MOJA NA WANAOWAPIGA WANDISHI WA HABARI
Baraza la habari Tanzania (MCT) limesema kuwa kuanzia sasa litakuwa likiwapeleka mahakamani watu wanaoripotiwa kuwazuia, kuwanyanyasa na kuwapiga waandishi wa habari wawapo katika majukumu yao.
Hayo yamezungumzwa leo na Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Bw.Kajubi Mukajanga alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kupinga jinai dhidi ya wanahabari yaani(International Day to end impunity for crime Against journalists) ambapoamewataka waandishi wote wa habari nchini kuanzia sasa kuhakikisha wanapata taarifa sahihi za watu wanaowazuia au kuwafanyia vitendo viovu wawapo katika majukumu yao ili kuwepo na taarifa za uhakika kuwezesha kesi kufunguliwa ikiwa Lengo ni kumshitaki jahili mmoja mmoja ili awajibike kwa matumizi mabaya ya madaraka au kwa unyanyasaji
Aidha Bw.Mukajanga amewakumbusha viongozi wa vyombo vya habari hususani wamiliki,watendaji wakuu na wahariri wajibu wao wa kuwalinda waandishi wao na kuzingatia usalama wao.
Kwa upande wao baadhi ya wandishi wa habari kutoka vyomba vya habari hapa nchini ambao wameomba majina yao yasitajwe wala wanapotoka wameiambia Salvahabari kuwa bado wanakumbana na changamoto mbalimbali ikiwemo sheria ambazo haziwapi uhuru wa kufanya kazi zao ipasavyo
Siku ya maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Kupinga Jinai Dhidi ya Wanahabari, yaani International Day to End Impunity for Crimes Against Journalists huadhimishwa kila Novemba 2 na ilipitishwa kwa Azimio la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa katika kikao chake cha 68 mwaka 2013.
Na James Salvatory
Post a Comment