EU YAMWAGA BILIONI 130 TANZANIA
Umoja wa Ulaya (EU) umetoa msaada wa kiasi cha Euro Milioni 50 ambazo ni sawa na takribani shilingi bilioni 130 za kitanzania kwa ajili ya miradi ya usambazaji wa Umeme Vijijini inayotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA)
Akizungumza Leo jijini dar es salaam kabla ya kusaini makubaliano hayo Katibu mkuu wa wizara ya fedha nchini Dotto James amesema kuwa mpka kufikia mwaka 2020 vijiji vyote nchini vitakuwa vimeunganishwa na huduma ya umeme kupita mradi wa umeme vijijini wa Rea
Aidha amesema kuwa toka mradi wa Rea unzishe mwaka 2008 vijini ambavyo vilikuwa vimeunganishwa ilikuwa 2% tu ya idadi yote ya Vijini vipatavyo 12000 Wakati kwa mwaka huu wa 2017 ni 49.3% ya vijini umeunganishwa umeme Huku asilimia 10 ya wananchi kitaifa walikuwa wanapata Umeme lakini hadi kufikia Desemba, 2016 ni asilimia 67.5 wanapata Umeme wa uhakika.
Kwa upande wake Kamishna wa Maendeleo wa Umoja wa Ulaya (EU), Neven Mimica amesema kuwa Umoja huo unatambua juhudi zinazofanywa na Serikali kupitia Wizara ya Nishati katika usambazaji wa Umeme vijijini hivyo wapo tayari kuisaidia Serikaliili iweze kutimiza malengo ya Dira ya Maendeleo ya Taifa yenye lengo la kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa nchi ya kipato cha kati ifikapo mwaka 2025.
Kwa upande wao baadhi ya wakazi wa jiji la dar es salaam wameishauri serikali kuboresha kwanza huduma za umeme ikiwemo umeme kuwa wa uhakika na wenye nguvu wa kusukuma mitambo yote kwenye hivyo vijiji watakavyopeleka umeme huo
Na James Salvatory
Post a Comment