SHANNA-MFUGAJI AUAWA KWA KUCHOMWA KISU KWENYE ULEVI NA KG 7,500 ZA BANGI ZAKAMATWA PWANI
Kamanda wa Polisi Mkoani Pwani
(ACP)Jonathan Shanna ,akizungumza na baadhi ya waandishi wa habari
(hawapo pichani)ofisini kwake Kibaha.
Mwamvua Mwinyi
…………………
Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
Mfugaji Lemandra
Kishakwi (35)mkazi wa Chamakweza ,Chalinze mkoani Pwani ,ameuawa kwa
kuchomwa kisu maeneo mbalimbali ya mwili na mwenzake Niniyay Silongoy
chanzo kikidaiwa ni ulevi.
Aidha jeshi la polisi mkoani hapo ,limekamata bangi gunia saba zikiwa kwenye mifuko ya salfet ambazo zina uzito wa kg 7,500 .
Kamanda wa polisi
mkoa wa Pwani ,(ACP)Jonathan Shanna akielezea tukio la mauaji alisema
limetokea octoba 18 majira ya saa 11.30 jioni,huko Chamakweza.
Alisema kuwa
,Lemandra ambae ni (mmasai )mfugaji aliuawa kwa kuchomwa kisu maeneo ya
kwapa la kushoto ,shingoni na mkono wa kulia wakati wakiwa kwenye ulevi.
Kamanda Shanna
,alielezea mtuhumiwa alikimbia kusikojulikana baada ya kufanya tukio
hilo na polisi inaendelea na juhudi za kumtafuta .
Mwili wa marehemu umekabidhiwa kwa ndugu wa marehemu mara baada ya uchunguzi wa daktari kukamilika.
Akielezea kuhusiana
na tukio la kukamata bangi ,kamanda Shanna alisema askari wakiwa doria
eneo la Kwamatias Kibaha ,walipata taarifa kuwa kuna ajali ya gari
no.T847 DHT aina ya I.S.T.
“Walipofika eneo la
tukio waliwaokoa majeruhi Gudluck Kundaeli Mbowe (24)mkazi wa Kiwalani
jijini Dar es salaam aliyekuwa dereva wa gari hilo na Ally Mtena (28)
mkazi wa Gongolamboto “
“Wakati wanapekua gari hilo waliikuta ikiwa na gunia saba za bangi zikiwa kwenye salfet ,zenye uzito wa kg 7,500.:”;
Kamanda huyo wa polisi mkoani humo ,alibainisha watuhumiwa wamekamatwa ili kuweza kuchukuliwa hatua za kisheria .
Post a Comment