Header Ads

header ad

JUKATA KUFANYA MAANDAMANO NCHI NZIMA



Jukwaa la Katiba nchini (JUKATA) limesema litafanya maandamano  nchi nzima   siku ya tarehe 30 ya mwezi huu yakiwa na lengo la kudai katiba mpya na kuleta hamasa kwa wananchi kuendelea kushiriki  kwenye mchakato ya kidemokrasia hapa nchini


Akitangaza Maandamano hayo Leo jijini Dar es salaam wakati Wa mkutano na waandishi Wa Habari,Mkurugenzi Mtendaji Wa (JUKATA),Hebron Mwakagenda amesema baada ya mkutano Mkuu wa Jukwaa hilo uliofanyika mkoani Dodoma mwisho mwa wiki iliyopita wamezimia kufanya maandamano nchi mzima yenye lengo la kudai katiba mpya huku maandamano hayo kwa upande Wa Mikoa  mingine nje ya Dar  yatafanyika kila wilaya.

"Tumeazimia kufanya maandamano siku ya tarehe 30 ya mwezi huu, katika ngazi ya  kitaifa ambayo yatafanyika Jijini Dar es Salaam yakianzia ofisi za JUKATA  hapa Mwenge Saa nne asabuhi na yatahitimishwa katika viwanja vya mnazi mmoja"  Mkurugenzi Mtendaji Wa (JUKATA),Hebron Mwakagenda

No comments

Powered by Blogger.