Header Ads

header ad

WADANGANYIFU WA MITIHANI WAONYWA

Baraza la mtihani la Tanzania limewataka wasimamizi,watahiniwa,wamiliki wa shule pamoja na  wananchi wote  kutojihusisha na vitendo vyovyote vya udanganyifu wa Mtihani wa kumaliza Elimu ya msingi unaoanza hapo kesho nchi nzima.


Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Salaam Katibu Mtendaji wa baraza hilo Dkt.CHARLES MSONDE amesema jumla ya watahiniwa waliosajiliwa kufanya mtihani ni 917,072 kati yao wavulana ni 432,744 sawa na asilimia 47.19 na wasichana ni 484,328 sawa na asilimia 52.81 huku kwa Mwaka jana watahiniwa waliosajiliwa kufanya mtihani huo walikuwa 795,761.

 Aidha amesema maandalizi yote kwa ajili ya mtihani huo yamekamilika ikiwa ni pamoja na kusambazwa kwa karatasi za mtihani, fomu Maalum za OMR za kujibia mtihani na nyaraka zote muhimu zinazohusu mtihani huo katika halmashauri na manispaa zote nchini.

Baadhi ya wazazi wa wanafunzi wanotarajiwa kufanya mtihani kesho ambapo wamewaomba wanafunzi na wasimamizi kufuata kanuni zilizoelekezwa na baraza la mtihani Tanzania

No comments

Powered by Blogger.