FAO YALETA NEEMA NCHINI KATIKA SEKTA YA KILIMO
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, (FAO), José Graziano da Silva (Kulia), akimpongeza Waziri wa kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe Dkt Charles Tzeba mara baada ya kuelezea taarifa mbalimbali zihusuzo wizara hiyo. leo Jumanne Septemba 5, 2017.
Waziri wa kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe Dkt Charles Tzeba akizungumza kabla ya kumkaribisha Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, (FAO), José Graziano da Silva, kuzungumzia ujio wake nchini na ushirikiano baina ya FAO na serikali ya Tanzania. leo Jumanne Septemba 5, 2017.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, (FAO), José Graziano da Silva, akizungumzia na wataalamu mbalimbali katika Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi juu ya ujio wake nchini na ushirikiano baina ya FAO na serikali ya Tanzania. Kulia kwake ni Waziri wa kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe Dkt Charles Tzeba. leo Jumanne Septemba 5, 2017.
Wataalamu mbalimbali katika Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi wakimsikiliza kwa makiniMkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, (FAO), José Graziano da Silva.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, (FAO), José Graziano da Silva (Kushoto) akiteta jambo na mwenyeji wake Waziri wa kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe Dkt Charles Tzeba mara baada ya kutembelea ofisini kwake.leo Jumanne Septemba 5, 2017.
Waziri wa kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe Dkt Charles Tzeba akipokea simu 50 kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, (FAO), José Graziano da Silvakwa ajili ya wataalamu wa kilimo kuzitumia kukusanya taarifa mbalimbali na kuziwasilisha kwa jamii. leo Jumanne Septemba 5, 2017.
Waziri wa kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe Dkt Charles Tzeba akionyesha moja ya siku kati ya 15 alizokabidhiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, (FAO), José Graziano da Silva kwa ajili ya wataalamu wa kilimo kuzitumia kukusanya taarifa mbalimbali na kuziwasilisha kwa jamii. leo Jumanne Septemba 5, 2017.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, (FAO), José Graziano da Silvaakiteta jambo na Waziri wa kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe Dkt Charles Tzeba mara baada ya kupokea zawadi. leo Jumanne Septemba 5, 2017.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, (FAO), José Graziano da Silvaakipokea zawadi ya vinyago kutoka kwa Waziri wa kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe Dkt Charles Tzeba mara baada ya mazungumzo ya kikazi kumalizika. leo Jumanne Septemba 5, 2017.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, (FAO), José Graziano da Silvaakiwaaga watendaji wa wizra ya kilimo Mifugo na Uvuvi mara baada ya kumalizika kwa mkutano akiwa na mwenyeji wake Waziri wa kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe Dkt Charles Tzeba. leo Jumanne Septemba 5, 2017.
Picha ya pamoja kati ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, (FAO), José Graziano da Silva (Aliyeketi kwenye kiti kulia), Waziri wa kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe Dkt Charles Tzeba, Katibu Mkuu wizara ya kilimo Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Dkt Maria mashingo na wataalamu wengine kutoka FAO na Wizara ya kilimo.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, (FAO), José Graziano da Silva, leo amefanya mazungumzo na Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye masuala makuu yanayohusiana na uhakika wa chakula na maendeleo ya kilimo, ikijumuisha juhudi za FAO kitaifa na kikanda huku yamejadiliwa mambo mengine yanayohusiana na ushirikiano kati ya Tanzania na FAO.
Akizungumza na Wandishi wa habari mara baada ya mazungumzo hayo Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Dkt Charles Tzeba alisema kuwa ujio wa Bw. Graziano da Silva nchini unaakisi ushirikiano bora uliopo kati ya Tanzania na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, (FAO) ambapo hivi karibuni ILO walisaidia katika kuandaa mpango wa kilimo kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi kwa kutoa fedha ya kutengeneza programu ya kutoa maarifa kwa wananchi ya namna ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi katika kilimo.
Aidha amesema Dkt Tzeba FAO wametoa simu 50 na Kompyuta 15 kwa wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi kwa ajili ya wataalamu wake kuwa na urahisi wa kukusanya taarifa na kuzifikisha kwa jamii.
Katika ziara hiyo Bw. Graziano da Silva atafanya mazungumzo na viongozi waandamizi wa Serikali, na anatarajiwa kukutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein sambamba na Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi wa Zanzibar, Hamad Rashid Mohamed huku Ziara hiyo ikijili wakati FAO ikiadhimisha miaka 40 toka kuanza shughuli zake hapa Tanzania Hafla ambayo itahudhuriwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bi. Samia Suluhu Hassan.
Post a Comment