MAGUFULI "KUMWACHIA KIJITI" RAIS MUSEVEN EAC.
Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli anatarajia kumaliza muhula wake kama Mwenyekiti wa jumuiya ya Afrika mashariki kesho jumamosi may 20,2017 na kumwachia rais wa Uganda,Yoweri Museven kuwa Mwenyekiti mpya wa jumuiya hiyo kwa mwaka 2017/2018
Akizungumza jijini Dar as salaam katika mkutano wa 34 wa baraza la mawawaziri na viongozi mbali mbali wa jumuiya ya afrika mashariki jana waziri wa mambo ya Nje na ushirikiano wa afrika mashariki,kikanda na kimataifa Balozi Augustine Mahiga amesema baada ya Tanzania kuwa wenyeji wa jumuiya hiyo umefika wakati wa kuikabidhi nchi nyingine ambapo nchi ya Uganda ndo itakuwa ikiiongoza jumuiya hiyo kwa mwaka 2017/2018 ambapo itakabidhiwa jijini Dar es salaam kwenye mkutano wa wakuu wa nchi za EAC.
Aidha Balozi Mahiga amesema kuwa katika kipindi ambacho Tanzania imekuwa mwenyeji wa jumuiya hiyo imetatua changamoto mbali mbali sambamba na kufanikisha nchi ya Sudan kujiunga na umoja huo.
Tanzania ilichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa jumuiya ya afrika mashariki mnamo mwaka Jana ikiwa imeongoza katika vipindi viwili baada ya rais mstaafu Jakaya Kikwete kumaliza muda wake mwaka 2016 hivyo wajumbe wa umoja huo wakampitisha rais Magufuli kuwa Mwenyekiti wa EAC na kuifanya nchi ya Tanzania kuongoza kwa mihula miwili mfululizo jumuiya hiyo
Post a Comment