MAKONDA,ATOA NEEMA KATIKA SEKTA YA AFYA
Serikali ya Tanzania kupitia ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam imetoa siku 5 kwa wananchi wa Mkoa wa Huo kujitokeza siku ya jumatano tarehe 6 Septemba mwaka huu katika viwanja mnazi mmoja ,kupima afya zao.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda, ambapo amesema serikali yake imeona ni vyema kuendeleza huduma ya afya, hivyo wananchi wote wa mkoa huo wametakiwa kujitokeza kuanzia asubuhi mpaka jioni kupima ili kujua afya zao.
“Kitendo chaa kupima afya kinatoa unafuu wa kujua namna gani ya kujipanga katika sekta nzima ya afya ilikupunguza vifo,kuna magonjwa mengine ambayo huwezi kuyafahamu mpaka upimwe alafu ugundulike kinachokusumbua,na wakati mwengine ukichelewa kupatiwa huduma, huwapa shida kubwa madaktari na hata wewe mwenyewe unaweza kupoteza maisha yako kwa kuchelewa kujua kinachokusumbua”Alisema Makonda.
Ameleeza kitendo hiki kinamhamasisha mwananchi kuwa na utamaduni wa kupima afya ambapo kufanya hivyo kunarahisisha kuepusha gharama, na kuondokana na na Magonjwa ambayo ungeweza kuyaepuka endapo utapata taarifa mapema.
Magonjwa yatakayopumwa ni pamoja na kansa,tezi dume,macho,meno,na kila aina ya ugonjwa .
Aidha Makonda amesema kutokana na changamoto ya ugonjwa wa homa ya ini , madaktari wanajipanga kuona namna gani wanaweza kushughulika na ugonjwa huo.
Amefafanua kwa lengo lake ni kuona hakuna mwananchi wake ambae atakufa kwa kukosa huduma ya afya ispokuwa mgonjwa afe kwa mapenzi ya Mungu.
Upimaji huo utakuwa ni bure bila tozo ya aina yeyote,ambapo wataalamu zaiidi ya mia mbili watakuwa tayari kwa kutoa huduma kwa wananchi watakao jitokeza.
Nae Mganga mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Bi. Grace Magembe amesema zoezi hilo limeshirikisha wadau kutoka serikalini na wengine wa taasisi binafsi ambapo kwa upande wa Serikali, madktari kutoka hospitai ya Taifa Muhimbili,jakaya Kikwete,Ocean Road,Amana ,Mwananyamala, Temeke, wengine ni TMJ,LEGENCY,AGAKHAN,IMILIFE,Chama cha watoa huduma binafsi,CCP MEDICINE,DAMU SALAMA,Shirikaa la MDH,Shirika la bima ya afya NHIF,KAIRUKI,SANITAS.N.K
Amesema wagonjwa wote watahudumiwa na wale watakao stahili kupata rufaa atapewa kuwakati unaotakiwa.
Post a Comment