WAZIRI WA ARDHI AENDELEA KUTATUA KERO NA KUTOA TAHADHARI YA UTAPELI WA NYARAKA ZA UMILIKI
Baadhi ya Wazee wa wilaya ya Ilala wakiwa katika foleni nje ya Ofisi ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Mhe. William Lukuvi, wakisubiri kuwasilisha Kero zao.
Baadhi ya Wakazi wa wilaya ya Ilala waliofika Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuwasilisha Kero zao kwa Mhe. William Lukuvi.
………………………………………………………….
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Mhe. William lukuvi ameendelea na zoezi la kusikiliza kero za wananchi mkoani Dar es salaam ,ambapo leo alikuwa akisikiliza kero za wananchi wa wilaya ya Ilala.
Zaidi ya Wananchi elfu moja wamesikilizwa kero zao katika zoezi hilo. Aidha, Mhe. Waziri ametoa tahadhari ya aina nyingine ya utapeli; ambapo ameeleza kuwa matapeli wamekuwa wakighushi barua za toleo/ Offer Letter za wananchi.
Mhe. Lukuvi amesema kuwa imebainika kuwa kuna Matapeli ambao wamekuwa wakishirikiana na maafisa ardhi ambao sio waaminifu na wamekuwa wakitumia barua za toleo za wananchi wa kipato cha chini kwa kutengeneza barua za toleo nyingine kwa viwanja ambavyo vimeshakwisha milikishwa.
Amesema matapeli hao hutumia majani ya chai ili kuchakaza barua hizo ili zionekane chakavu kuliko zile za awali.
Aidha; Wananchi waliohudumiwa leo wamepongeza hatua za Mhe. Lukuvi katika kutatua changamoto zinazowakabili kwani wamekuwa wakiteseka kwa muda mrefu.
Post a Comment