WATU WATATU WAUWAWA DAR
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limesema limeokota miili ya watu wawili kando ya fukwe ya bahari ya hindi eneo la oystarbay na raia mmoja wa afrika ya kusini aliyejulikana kwa jina la Wayne Lotter miaka 52, mkurugezi wa Palm conservation foundation akiwa ameuwawa na watu waliozaniwa kuwa majambazi katika makutano ya barabara ya Haile Slassie na kaole Masaki kwa sasa bado wanaendelea na uchunguzi.
Akizungumza na mwandishi wa habari habari Leo jiji dar es salaam kaimu Kamanda wa polisi kanda maalumu ya dar es salaam Lucas mkondya amesema kuwa bado wanaendelea kuchunguza miili hiyo na kwa sasa iko katika hosptali ya taifa ya muhimbili na watatoa taarifa baada ya uchunguzi kukamilika
Aidha mkondya amesema kuwa wamefanikiwa kuwakamata jumla ya watuhumiwa 150 ikiwemo wapiga debe katika stendi za mabasi kwa makosa ya kubughudhi abiria katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam.
Katika hatua nyingine Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dsm limefanya misako na kufanikiwa kuwakamata jumla ya watuhumiwa 167 kwa makosa mbalimbali ikiwemo kupatikana na madawa za kulevya, unyanga’nyi wa kutumia silaha/ nguvu, utapeli, wizi kutoka maungoni, kucheza kamari kuuza pombe haramu ya gongo, kupatikana na bhangi katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam .
Stendi za mabasi ambazo jeshi la polisi limefanya msako na kuwakamata waarifu ikiwemo wapiga debe ni pamoja na Ubungo wamekamatwa watuhumiwa 39, posta watuhumiwa 12, Ferry watuhumiwa 7, Tegeta watuhumiwa 12, Tandika watuhumiwa 16, Mnazi mmoja watuhumiwa 6, Kituo cha daladala Stesheni watuhumiwa 5,Temeke Sterio 7,Gerezani 16, Manzese watuhumiwa 12, Bunju B watuhumiwa 8, Kijiwe samli watuhumiwa 2 na Buguruni watuhumiwa 3. Aidha watuhumiwa wote watapelekwa mahakamani ili kujibu mashtaka yanayowakabili.
Na James Salvatory
Post a Comment