Header Ads

header ad

SERIKALI YAPATA GAWIO LA SHILINGI BILIONI 19.5 KUTOKA BENKI YA CRDB


01
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Dotto James akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Ndogo za wizara hiyo jijini Dar es salaam kabla ya kupokea mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi Bilioni kumi na tisa na milioni mia tano 19.5 kama gawio lake kutoka benki ya CRDB wakati benki hiyo ilipokabidhi gawio hilo kwa serikali, Serikali inamiliki asilimia 21 ya hisa za benki ya CRDB na ndiyo yenye hisa nyingi zaidi kati ya wanahisa wote, Kulia katika picha ni Dk. Charles Kimei Mkurugenzi Mkuu wa Benki hiyo.

1
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Dotto James akimsikiliza Dk. Charles Kimei Mkurugenzi Mkuu wa Benki wa benki ya CRDB wakati akizungumza katika hafla hiyo kabla ya kukabidhi hundi ya gawio la faida kutoka benki hiyo kwa serikali, Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya CRDB Bw.Ally Hussein Laay.
3
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Dotto James akipokea mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi Bilioni kumi na tisa na milioni mia tano 19.500.000.000 Kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya CRDB Bw.Ally Hussein Laay kama gawio serikali  kutoka benki ya hiyo na katikati ni Kaimu Balozi wa Ubalozi wa Denmark nchini Tanzania Camilla Christensen
45
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Dotto James akimpongeza Mkurugenzi Mkuu  wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei mara baada ya kupokea hundi hiyo.
6
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Dotto James akipiga picha ya pamoja na wakuu wa benki ya CRDB pamoja na watendaji wakuu kutoka Wizara ya Fedha na Mipango mara baada ya kupokea hundi hiyo katikati ni Kaimu Balozi wa Ubalozi wa Denmark nchini Tanzania Camilla Christensen.
7
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Dotto James akipiga picha ya pamoja na wakuu wa benki ya CRDB pamoja na watendaji wakuu kutoka Wizara ya Fedha na Mipango mara baada ya kupokea hundi hiyo katikati ni Kaimu Balozi wa Ubalozi wa Denmark nchini Tanzania Camilla Christensen.

No comments

Powered by Blogger.