AGA KHAN KUSAIDIA MRADI WA WOMEN FOR WOMEN
NA
MWANDISHI WETU
Hospitali ya Aga Khan kwa kushirikana na wadau mbalimbali
wanatarajia kuanza kuwafanyia upasuaji wanawake 40 wanaosubuliwa na ugonjwa wa kukomaa
vioungo mwa mwili.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Daktari Bigwa Mkuu wa Upasuaji
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dkt Edwin Mrema, amesema kuwa ugonjwa huo unatokana
na muhusika kupata ajali yoyote ikiwemo moto pamoja na kufanyiwa ukatili katika
jamii.
Dkt Mrema amesema kuwa utaratibu wa kuwapata wangonjwa hao, kutakuwa
na kambi kwa ajili ya kuwaangalia wangonjwa wenye uitaji zaidi kwa ajili ya kufanyiwa
upasuaji wa aina hiyo.
Amesema kambi hiyo inatarajia kufanyika Septemba 16 mwaka
huu kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 8 mchana katika hospitali ya Aga Khan
iliyopo jijini Dar es Salaam.
“Mwaka huu tumeamua kuweka kambi kwa ajili ya kuhamasisha
watu wanaosumbuliwa na maradhi yanayotokana na moto au ajali na kusababisha
ukilema wa viungo vya mwili” amesma Dkt Mrema.
Akifafanua kuhusu mradi huo unaojulikana kwa jina ‘Women for
women’ Meneja Masoko na Mawasiliano, Ohyce Steven Lotha amesema kuwa kwa
wagonjwa waliopo Mikoani watalazimika kwenda katika vituo vya hospitali vya Aga
Khan kwa ajili ya kupigwa picha kasha kutwa jijini Dar es Salaama kwa ajili ya kuangalia
ukubwa wa tatizo.
Amesema kuwa wanafanya hivyo ili kuepuka usumbufu unaweza
kujitokeza kwa wagonjwa, kwani lengo leo ni kutafuta watu wenye uitaji wa
kufanyiwa upasuaji.
“Unakuta mtu anakuja Dar es Salaam baada ya kumpima unabaini
tatizo lake ni dogo na hawezi kufanyiwa upasuaji kwa hali hiyo ni usumbufu
mkubwa, ila tunaamini utaratibu huu utakuwa mzuri” amesema Lotha.
Hata hivyo amesema kwa uataribu wa gharama mgonjwa mmoja
anayefanyiwa upasuaji gyake Shillingi Milioni moja hadi tano, lakini wao
wamejipanga kutoa huduma hiyo bure pasipo kuwa na gharama yoyote.
Amesma kuwa gharamWETU
upasuaji kwa watu 40 ni zaidi ya Milioni 131 ambayo tayari wamejipanga kikamilifu kwa ajili ya kutekeleza jukumu hilo linalotarajiwa kufanyika Novemba 3 na 5 mwaka huu.
upasuaji kwa watu 40 ni zaidi ya Milioni 131 ambayo tayari wamejipanga kikamilifu kwa ajili ya kutekeleza jukumu hilo linalotarajiwa kufanyika Novemba 3 na 5 mwaka huu.
Mwaka wa jana walifanikiwa kuwafanyia upasuaji watu 32,
lakini kutokana na uhitaji wa huduma hiyo mwaka huu wameamua kuongeza idadi na
kufika 40.
Post a Comment