KAMANDA MAMBO SASA, RASMI DAR
Kamishana mpya wa Kanda maalumu ya Dar es salaam Kamishina mwandamizi wa Jeshi la Polisi Lazaro Mambo Sasa amewaomba wananchi kushirikiana na jeshi la polisi katika kuwafichua wahalifu wanaojificha jijini Dar es salaam.
Akizungumza leo na wanahabari katika mkutano wake wa kwanza wa kujitambulisha kwa wanahabari ,Mambo sasa ambaye ameteuliwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro kushika nafasi hiyo amesema kuwa amepanga mikakati kadhaa ya kupambana na vitendo vya uharifu ikiwemo vitendo vya wizi na kutekaji.
Aidha Mambo sasa amesema kuwa atahakikisha anatambua uwepo wa vyombo vya usalama,kushirikiana na madiwani na wabunge pamoja na maafisa watendaji wa mitaa na wanchi wote katika kupambana na vitendo vya uhalifu.
Akizungmzia kuhusu uchunguzi wa kulipuliwa kwa kampuni ya mawakili ya Immma Adviocates Kamishana huyo Mwandamizio wa Jeshi la Polisi Kandamaalumu ya Dar es salaam amesema ku uchunguzi bado unaendelea ila amewaonfya baadhi ya watu ambao wamelichukulia kisiasa tukio hilo na kuwataka waache kuwapotosha wananchi wakati uchunguzi wa kubaini waliyohusika na tukio hilo ukiendelea kufanyika.
Habari Xtra iliweza kuzungumza na mkazi wa jiji hili na hapa anataja vipambele ambavyo vimekuwa changamoto kubwa kwa jiji hili Kamishana huyo mpya aanze navyo ili .
Kamishna Msaidizi mwandamiziLazaro Mambosasa kabla hajateuliwa na Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi Simon Sirro kushika nafasi ya Kamanda wa Kanda maalumu ya Dar es salaam,amekuwa kamanda wa polisi Mkoa wa Dodoma,na pia ametumikia nyadhifa mbalimbali ndani ya jeshi hilo.
Post a Comment